Na Mwandishi Wetu
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Franklin Jasson Rwezimula Leo Julai 13 , 2023 amefanya ziara katika Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam kwa lengo la kujionea maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Kikanda cha Umahiri wa TEHAMA kitakachoitwa RAFIC .Akizungumza baada ya kuona Maendeleo ya Ujenzi Dkt. Franklin ameipongeza Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam ( DIT ) kwa hatua nzuri waliyofikia katika usimamizi wa Mradi huu mkubwa ambao una faida ndani na nje ya Nchi" Tunategemea Kituo hiki kitakua na FANI kubwa na zitakazofaidisha nchi Wanachama wa Afrika Mashariki , Nimeongea na wajenzi wamenipa ahadi kwanza mradi utakamilika kwa wakati yaani kuja kufikia mwezi wa pili Mwakani watakua wamemaliza kabisa "
" Kituo hiki kikikamilika kitasaidia kwanza kwa nchi kupata WATAALAMU wa mambo ya ICT na tunataka kujenga uwezo wa nchi kupata wataalam wenye ujuzi wa mambo ya ICT , Serikali yetu iko kwenye mapitio ya sera ya Elimu ya 2014 Tolea la 2023 ambapo mitaala inasisitiza Masomo ya Computer Sayansi ili Mwanafunzi akimaliza Sekondari awe na ujuzi wa KITEHAMA kwahiyo una imani Taasisi ya DIT itakua msaada Mkubwa katika hilo " Alimalizia
Akiuelezea Mradi huo, Mratibu wa RAFIC wa DIT, Dk. Joseph Matiko, anasema: “Ni mradi mkubwa wa miaka mitano ulioanza mwaka 2019, ambapo Benki ya Dunia imetoa Dola za Marekani milioni 16.25.
" Mradi wa RAFIC wa DIT unajikita katika uimarishaji wa stadi za kidigitali , hapa kuna stadi za msingi (basic skills) yaani kuhakikisha hata watu wa chini wanaweza kutumia kwa ufanisi vifaa vya kama simu katika shughuli zao. Pia, tuna ‘standard skills, ambapo hapa unapeleka umahiri kwenye mifumo rasmi ya elimu, mfano madaktari, waalimu n.k.Lakini pia kuna kundi la wabobezi. Wote wanahusika katika kuimarishiwa umahiri wao wa utumizi wa vifaa vya TEHAMA,”Aidha Dkt. Matiko amemalizia kwa kumpongeza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Viongozi alioambatana nao kwa kuja kushuhudia na kuchangia maoni kuhusu maendeleo ya Mradi huu Mkubwa .
DKT. RWEZIMULA AFANYA ZIARA DIT , UKAGUZI WA MAENDELEO YA MRADI WA RAFIC
Reviewed by Adery Masta
on
July 13, 2023
Rating:
No comments: