Na Adery Masta.
Tigo na Samsung wanakukaribisha kwenye banda lao katika Viwanja vya saba saba ili ujipatie huduma na zawadi kibao ikiwemo SIMU ZA MKOPO aina ya SAMSUNG AO4 na SAMSUNG AO4s mkopo ambao pia utaweza kuupata kwa kutembelea maduka ya TIGO au SAMSUNG hata baada ya MAONESHO SABASABA .
SIMU KWA ELFU 70: " Tigo tukishirikiana na wadau wetu SAMSUNG tunawaletea WATANZANIA simu aina AO4 na AO4s kwa MKOPO , simu ambazo kama kampuni ya Kidigitali tunazileta kwa ajili ya kurahisisha maisha , Mteja atahitaji kulipia kianzio cha Tsh. Elfu 70 kwa A04 na Elfu 90 kwa A04s baada ya hapo atakua analipia kidogo kidogo ndani ya MWAKA MZIMA , Lakini pamoja na kuwakopesha hatujawaacha wateja wetu hivihivi tutawapa na GB hadi 91 BURE mwaka Mzima " - Imelda Edward - Meneja wa Vifaa vya Intaneti kutoka Tigo.
AO4 na AO4s NI BORA SANA : " Pamoja na kuwakopesha wateja wetu simu hizi zina WARRANTY ya Miezi 24 ambapo mteja akikuta zina tatizo lolote anaweza kubadilishiwa BURE , Zina Kamera kali sana na zinakaa na chaji muda mrefu , Karibuni sana katika banda letu hapa SABASABA na Katika maduka ya Tigo na SAMSUNG nchi nzima mjitapie simu bora kutoka SAMSUNG ". - Edwin Byampanju - Msimamizi wa Mauzo SAMSUNG Tanzania.
Kwa maelezo zaidi kuhusu OFA hizi za TIGO NA SAMSUNG Tafadhari tembelea mitandao yao ya Kijamii au Maduka yao nchi nzima.
JINSI YA KUPATA MKOPO WA SIMU ZA SAMSUNG AO4 na AO4s , GB 71 BURE KUTOKA TIGO
Reviewed by Adery Masta
on
July 06, 2023
Rating:
No comments: