test

ASKARI POLISI 4,499 WAHITIMU MAFUNZO CCP-MOSHI

 Jumla ya Askari Polisi 4,499  wamepandishwa vyeo vya uongozi mdogo cheo cha Sagini Meja (SM) na Coplo (CPL) baada ya kuhitimu mafunzo ya miezi mitatu kutoka vyeo vya awali Sagni (SGT) na Polisi Kontebo (PC) yaliyokuwa yakifanyika katika Kambi ya Kilele Pori katika shule ya Polisi Moshi mkoani Kilimanjaro. 


Akizungumza na wahitimu hayo pamoja na wananchi waliohudhuria ufungaji wa mafunzo hayo, Naibu waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo amewapongeza wahitimu hao kwa kufuzu na kupandishwa vyeo na umahiri mkubwa walio onesha katika gwaride na maonesho ya mbinu za medani. 


"Mmemaliza kipindi kizuri na nimejionea ukakamavu wenu na umahiri mkubwa mlionao, ni imani yangu na watanzania kuwa mtakwenda kutenda haki na kuimarisha ulinzi kwenye himaya zenu bila kuonea mtu hasa kuacha ukamataji wa kutumia nguvu alisema Sagini.


Aidha Mhe. Sagini amempongeza Mhe. Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. @samia_suluhu_hassan kwa kuwawezesha vyombo vya Usalama kufanya mafunzo mbalimbali na kuwapandisha vyeo pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi kwa kulisimamia Jeshi hilo na kuhakikisha Askari wanapata stahiki zao. 


Kufuatia Askari Polisi 55 kufeli katika mafunzo hayo Mhe. Sagini amelishauri Jeshi la Polisi kuwa na utaratibu wa kurudia mitihani kwa wahitimu wanaofeli mitihani ya mwisho ambayo inapelekea kukosa cheo. 


"Wahitimu hawa wameacha familia zao kwa ajili ya kutafuta cheo, anapomaliza leo na ukamwambia amefeli unamvunja moyo, nawashauri mkatazame upya utaratibu huu ikiwezekana kuwe na utaratibu wa kurudia mitihani kama utaratibu wa Nacte" alisema.


 Aidha, Naibu Kamishna wa Polisi Mary Nzuki ambaye alimwakilisha Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura  amewataka wahitimu hao kuhakikisha wanatumia elimu na utaalamu walioupata katika kudhibiti uhalifu katika maeneo yao.


Akizungumza kuhusu waliofeli kurudia mitihani ,Afande Nzuki amesema kuwa kulingana na Jeshi la Polisi,wanafunzi waliofeli  55 hawatapata promosheni ya kupandishwa vyeo hadi pale watakapo hudhuria mafunzo kwa mara nyingine na kufaulu.@polisi.tanzania  @policetanzania


ASKARI POLISI 4,499 WAHITIMU MAFUNZO CCP-MOSHI ASKARI POLISI 4,499 WAHITIMU MAFUNZO CCP-MOSHI Reviewed by VISIONMEDIA on September 07, 2023 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.