test

DC-MBULU ASISITIZA UMUHIMU WA MAADILI, MAARIFA NA STADI ZA MAISHA KWA VIJANA.

 *📍TLAWI - MBULU 🗓 SEPT 29, 2023.*                           


 



Mkuu wa wilaya ya Mbulu Komred Kheri James, mapema leo amewahimiza wazazi na jamii kwa ujumla kutumia fursa ya mazingira bora ya elimu yaliopo, kushirikiana na Walimu kuhakikisha Wanafunzi wanapata Elimu bora, Maadili na ujuzi wa kujitegemea kiuchumi.         


Komred Kheri James ameyasema hayo mapema leo katika Mahafali ya 17 ya Shule ya Sekondari Tlawi iliopo katika Halmashauri ya Mji wa Mbulu.                          


Komred Kheri James ametumia nafasi hiyo kuwahimiza Wanafunzi kujiandaa na kufanya vizuri katika mitihani yao na amewasihi wazazi kuwa Karibu zaidi kimalezi na watoto wao katika kipindi cha baada ya mitihani ili kuepuka madhara ya mmomonyoko wa maadili na matendo ya uharibifu.                                 



Kwa upande wa maendeleo ya sekta ya elimu, Komred Kheri James ameeleza kuwa Serikali ya awamu ya Sita Chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanikiwa kuleta zaidi ya shilingi bilioni moja na milioni mia mbili kwa lengo la kuboresha na kuimarisha miundombinu katika Shule za Sekondari za Halmashauri ya Mji wa Mbulu na itaendelea kufanya hivyo ili kuboresha elimu nchini.       


Mahafali ya 17 ya Shule ya Sekondari Tlawi, Imehudhuriwa pia na viongozi, Wananchi, Watumishi na Wazazi ambao kwa pamoja wamepata fursa ya kuwatakia heri wahitimu wa mwaka huu.                     



 *#Kwapamoja, Tunaijenga Mbulu yetu.*

DC-MBULU ASISITIZA UMUHIMU WA MAADILI, MAARIFA NA STADI ZA MAISHA KWA VIJANA. DC-MBULU ASISITIZA UMUHIMU WA MAADILI, MAARIFA NA STADI ZA MAISHA KWA VIJANA.  Reviewed by VISIONMEDIA on September 30, 2023 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.