Na Mary Margwe, Geita
Shirika la Uwakala na Meli Tanzania ( TASAC ) ni Shirika la Umma lililo chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, lilianzishwa Kwa mujibu wa sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania sura 415 na kuanzia kutekeleza majukumu yake kuanzia februari 23, 2018 baada ya Tangazo la Serikali ( G.N.Na.53 lililotangazwa februari 16, 2018.
Hayo yamebainishwa Jana na Afisa Uhusiano kwa Umma ( TASAC ) Amina Miruko, wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea katika Banda hilo.
Miruko amesema TASAC imekua ikifanya kazi katika maeneo 17, lakini kutokana na mabadiliko ya sheria ikapelekea kupunguziwa majukumu na kufanya kazi takika maeneo matano (5)
" Miongoni mwa maeneo haya ni pamoja na makinikia, upuri, ama Mashine mbalimbali zinazotumika katika uchimbaji wa Madini na migodini, pia ni risaha na virupuzi na viumbe hai hususani wanyama pori" amesema Miruko.
Afisa Udhibiti Huduma za Bandari ( TASAC ) Victoria Miyonga amesema TASAC ilianzishwa ili kudhibiti na kusimamia Sekta ya usafiri wa Majini ( Bahati, Mabwawa, miito) ambayo awali ilikua ikidhibitiwa na Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa nchi kavu na Majini ( SUMATRA )
Miyonga amesema TASAC kama wadhibiti huduma ya Bandari na usafiri wa usafiri wa njianya maji wanashughulika na cheni nzima ya usafirishaji kuanzia yule anayesafirisha mizigo na yule anayehakiki mizigo kwenye shehena .
Afisa Masoko Mwandamizi (TASAC) Martha Kelvin akizungumzia uwepo wao katika Maonyesho ya 6 ya Kimataifa na Teknolojia ya Madini Geita mwaka 2023 amesema wametoa elimu ya TASAC pamoja na kuwaelelezea wananchi majukumu ya TASAC.
" Jukumu mojamla TASAC ni kuhakikisha kwa upande wa Madini wanasafirisha vifaa na makinikia ambayo yanatumika katika Uchimbaji wa Madini" amesema Martha.
Hata hivyo Afisa Ugomboaji na Uondoshaji Shehena ( TASAC ) Nashon Midagwe amesema kuwa kuna bidhaa takribani 5 kama siraha, makinikia ,nyara za Serikali,wanyamapori, na kemikali zinazotumika katika uchimbaji wa Madini.
" Hizi ndio bidhaa tulizobaki nazo kama TASAC na tumekabidhiwa kisheria maana hazina ushindani" amesema Midagwe.
No comments: