Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini na naibu Waziri wa katiba na sheriaMh. Paulina Gekul Leo ametoa majiko ya Gesi 146 kwa wafanyabiashara wanaofanya Biashara ya Chakula (Mama lishe ikiwa ni sehemu ya kuwawezesha wafanyabiashara hao kutumia nishati mbadala
Akitoa Gesi hizo amewaambia kina mama hao kuwa wao kama wafanyabiashara wa Chakula wanapaswa kuungana na kuwa kitu kimoja ikiwa ni pamoja na kushirikishana katika Biashara Yao. Aidha ameeleza ugumu wa kufanya Biashara Huku akiwapongeza wafanyabiashara hao kwa kutokukata tamaa Huku akiendelea kuwatia moyo
Pamoja na hao ameendelea kuhamasisha wafanyabiashara hao kujitokeza katika kilele Cha kuzimwa kwa Mwenge wa Uhuru 2023 ambapo utazikwa tarehe 14.10.2023 Mkoani Manyara Jimbo la Babati Mjini kama
Utoaji wa majiko hayo ni mwendelezo wa majiko aliyoyatoa awali ambapo Julay mwaka 2022 alitoa majiko 500 Na Julay mwaka 2023 alitoa majiko 500
Zoezi Hilo pia limehudhuriwa na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Babati Mjini wakiongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake *EVA LUOGA* ambapo akitoa Salam Kiongozi huyo amesema ni kazi kubwa kupata Kiongozi anayejitoa Huku akiwasisitiza wafanyabiashara hao kuendelea kumuombea Mbunge wao *PAULINE GEKUL* kwa namna anavyojitoa kwa wananchi wake
Abrima Hussein
Katibu wa Mbunge Jimbo la Babati Mjini
No comments: