*ELIMU AFYA MALEZI NA MAZINGIRA*
Tahadhari ya Mvua Kubwa kupita kiwango ( ELNINO) , kuanzia October 2023
Lazima kuchukuwa tahadhari mapema kwa kuhakikisha njia za maji ni safi na hakuna uchafu unao zuia maji kupita
Tusafishe mitaro ya maji na kuchoma taka zote na kama kuna majani ama miti katika mitaro ya maji yaondolewe yote
Tuhahikikishe taka zote zinapelekwa katika madampu kuu ya taka ya miji yetu.
madampu yaliopo katika makazi ,soko , mjini n.k. taka zisikae kwa muda mrefu haraka haraka yatolewe na kupelekwa dampu kuu ili kuepuka magonjwa ya mlipuko kama cholera , kichocho n.k ..mvua zitakapo anza kunyesha na kuozesha taka katika makazi ya watu na maeneo yanayo wazunguka ndo huchochea magonjwa ya mlipuko
Hakikisha mitaro ya nyumbani kwako ni safi na weka mazingira yako ya nyumbani safi na salama kwa kukata majaini
Tutumie fursah katika kipindi hiki cha mvua kwa kupanda miti zaidi katika maeneo yanayo tuzunguka na pia kufanya kazi ya kilimo
Utunzaji wa mazingira na usafi wa maeneo yetu ni jukumu letu sote tutunze mazingira yatutunze .
Imetolewa na
Ndg. Ahmed Misanga
Mjumbe kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi -Mkoa wa Singida

No comments: