Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mwimbaji wa nyimbo za injili aitwaye Sifa Bonivanture Bujune, mwenye umri wa miaka 25 mkazi wa Isesye Jijini Mbeya kwa tuhuma za kuimba nyimbo za uchochezi dhidi ya serikali na kuziweka katika mitandao ya kijamii.
Akizungumza na vyombo vya vya habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya ACP Benjamin Kuzaga amesema mnamo tarehe 13/9/2023 jeshi la polisi lilimkamata mtuhumiwa huyo kwa makosa ya kuimba nyimbo zenye chuki na uchochezi dhidi ya serikali ya awamu ya sita na zisizo na maadili ya Kitanzania kisha na kuziweka katika mitandao ya kijamii na mitandao mingine.
ACP Kuzaga ameongeza ya kuwa mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na jeshi la Polisi kujua ni “Kwanini anatunga nyimbo hizo? nani amemtuma? na je yeye ni Mtanzania na kama si Mtanzania basi pia Jeshi la Uhamiaji litapata taarifa zake, lakin kama ni Mtanzania na anaendelea kufaidi mema yote ambayo yanafanyika katika Nchi hii kwa sasa chini ya Serikali ya awamu ya sita baada ya uchunguzi tutamfikisha Mahakamani kwa kosa la kuleta taharuki katika jamii”- RPC Benjamin Kuzaga
No comments: