test

TBS ELIMU KWA UMMA YAZIFIKIA WILAYA ZA MKOA WA TABORA

 Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linaendelea na Kampeni yake Ya kutoa Elimu Kwa Umma katika Ngazi za Wilaya ambapo hadi sasa Shirika hilo limetoa Elimu Kwa wananchi,Wafanyabiashara na Wajasiriamali Wadogo Ndani ya Wilaya 72 nchi nzima na Lengo likiwa ni kuzifikia Wilaya Zote nchini. 

Akizungumza Leo Septemba 19, 2023 katika Wilaya Ya Igunga mkoani Tabora Meneja Wa Uhusiano na Masoko TBS Bi.  Gladnes Kaseka amesema lengo la Shirika hilo ni kutoa Elimu Kwa Umma katika Ngazi za Wilaya zote.

" Kwa sasa TBS tumeamua kuwafikia Wajasiriamali ,Wafanyabiashara na wananchi katika Ngazi Za Wilaya ili  kuwapatia utaratibu unaotakiwa kwa ajili ya kupata alama ya Ubora na kusajili majengo ya Biashara ya chakula na Vipodozi ili kuepuka Usumbufu unaoweza kujitokeza lakini pia kuwasisitiza wananchi kuhakikisha bidhaa wanazozitumia kila siku zimethibitishwa ubora wake na TBS, kusoma muda wa mwisho wa matumizi sambamba na kuwajulisha njia wanazoweza kutumia kutoa taarifa wanapokutana na changamoto ya masuala ya ubora wakati wa manunuzi, ndio maana kwa hapa Igunga tumetembelea maeneo yenye mkusanyiko kama vile mnadani na masokoni ili kufikisha Elimu iyo kwa urahisi, kwahiyo Elimu hii ya Umma ipo katika ngazi ya Wilaya na hadi sasa TBS imezifikia Wilaya 72 , Leo tupo hapa Igunga vilevile tutaendelea katika wilaya za Uyui ,  Sikonge,  Kaliua na Tabora Manispaa ". amesema Bi.  Kaseka 

Nao Wajasiriamali na Wananchi kwa nyakati tofautitofauti wameipongeza TBS Kwa Elimu waliyoamua kutoa tena kwa kuwafuata katika maeneo yao maana imewafumbua Mambo mengi kuhusu umuhimu wa Viwango katika bidhaa wanazozizalisha na kuzitumia.



TBS ELIMU KWA UMMA YAZIFIKIA WILAYA ZA MKOA WA TABORA TBS ELIMU KWA UMMA YAZIFIKIA WILAYA ZA MKOA WA TABORA Reviewed by Adery Masta on September 19, 2023 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.