Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga, leo tarehe 22 Septemba, 2023 ameendelea na Ziara yake ya Kimkakati na kukagua Miradi Mbalimbali ya Afya ikiwemo Zahanati ya Gedamar, Zahanati ya Mwinkatsi na Kituo cha Afya Mamire ambayo iko katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati.
Pamoja na kufanya ukaguzi wa miradi hiyo, lakini pia RC. Sendiga amefanya mikutano ya hadhara katika Vijiji vya Mwinkatsi na Mamire na kusikiliza kero mbalimbali. Katika mkutano huo Mhe. Mkuu wa Mkoa Amewapa mwezi mmoja BAWASA kufanya mapitio ya bei (bili) zao ambazo zinalalamikiwa na wananchi.
Pia, RC. Sendiga ametoa maelekezo Mahsusi kwa Watendaji na Maafisa Tarafa wote wa Mkoa wa Manyara "Nikienda sehemu nikikuta kero naondoka na Watendaji Kijiji, Kata na Afisa Tarafa" kwani ni wajibu wao kupita na kusikiliza kero na matatizo kwa wananchi.
Aidha, Mhe. Mkuu wa Mkoa amesisitiza suala la Malezi bora kwa Vijana, Wazazi kuwafundisha watoto wao maadili mema na kuacha kuwatetea Watoto wao wanapotuhumiwa kufanya matendo maovu.
ZIARA YA RC SENDIGA BABATI DC
Reviewed by VISIONMEDIA
on
September 22, 2023
Rating:
No comments: