Mahakama ya Wilaya ya Babati Manyara imemtia hatiani na kumhukumu kifungo Cha Maisha Jela Mshitakiwa Mohamed Hayma (38) mkulima Mkazi wa Maisaka Babati. Akitoa hukumu hiyo imetolewa Tarehe 14 Septemba 2023 Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Babati Mheshimiwa Juma Mwambago amesema mahakama imeridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka na kumtia hatiani mtuhumiwa kwa kosa Hilo. Mshitakiwa amehukumiwa kifungo hicho ili iwe onyo na fundisho kwa jamii hususani wenye tabia za kufanya vitendo vya ukatili kwa watoto.
JELA MAISHA KWA KUMBAKA MTOTO WA MIAKA 6.
Reviewed by VISIONMEDIA
on
September 22, 2023
Rating:
No comments: