Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara linawashikilia watuhumiwa 23 kwa makosa mbalimbali ikwemo kukutwa na Bangi Kilo 9, lita 920 za Gongo na mitambo ya kutengenezea pombe hiyo
Akizungumza na waandishi wa habari mapema Leo 24 Oktoba, 2023 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Kamishna Msaidizi ( ACP) George Katabazi amesema operesheni hii ni ya kuanzia tarehe 11 Oktoba, 2023
Amewataja waliokamatwa ni Abdi Rajabu, Lobulu Slaa, Daudi Laizer, Laida Leheyi, Anthony Alphonce na wenzao 19
Aidha Katika operesheni hiyo Mali mbalimbali zililamatwa ikiwemo Pikipiki aina ya Kinglion Namba MC 174 CZX, simu 06, TV 02, Magodoro 06, na noti za fedha za kigeni
Katabazi amesema Operesheni hii ni endelevu na amewaomba wananchi kuendelea kishirikiana na Jeshi Hilo katika kuzuia na kutanzua Uhalifu.
No comments: