Moto ambao chanzo chake hakijajulika umeteketeza bweni la wasichana katika Shule ya Sekondar ya Marry Queen of Peace mjini Geita.
Janga hilo moto limetokea Saa 8:00 mchana Oktoba 23, 2023 wakati wanafunzi wakiendelea na shughuli za kawaida za kimasomo.
Licha ya kutekeza samani na mali za wanafunzi, moto huo pia imesababisha madhara ya mshtuko kwa baadhi ya wanafunzi.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na
Vokoaji Mkoa wa Geita, Hamis Dawa amesema askari wa jeshi hilo kwa kushirikiana na wadau wengine wamefanikiwa kuudhibiti moto huo
kabla ya kusababisha madhara makubwa.
"Tunaendelea na uchunguzi wa kina
kubaini chanzo cha moto huo," amesema Kamanda Hamisi
Katibu wa Askofu Jimbo Katoliki Geita inayomiliki Shule hiyo, Padri Yohane Mabula amesema moto huo umesababisha hasara ambayo thamani yake hiajajulikana hadi tathmini itakapofanyika.
Moto wateketeza Bweni la wasichana
Reviewed by VISIONMEDIA
on
October 24, 2023
Rating:
No comments: