test

BABATI DC YAPETA MIRADI YOTE, MWENGE WA UHURU 2023.

 



 Mwenge wa uhuru unaendelea na mbio zake mkoani Manyara ambapo katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati umekagua, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi tisa yenye thamani ya shilingi bilioni 1.9. 


Mradi mkubwa uliozinduliwa na mwenge wa uhuru na kupokelewa kwa shangwe na wananchi ni kituo cha afya Bashnet kilichojengwa na Serikali kwa zaidi ya shilingi milioni 602 kitakachohudumia wananchi zaidi ya 17,000 wa Tarafa ya Bashnet.


Mwenge wa uhuru pia umeridhia kufungua mradi wa Maji wa Kijiji cha Nar uliojengwa na Serikali kupitia wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) kwa zaidi ya shilingi milioni 208 utakaonufaisha Wananchi zaidi ya 4,630. 


Miradi mingine iliyotembelewa na mwenge wa uhuru katika halmashauri ya wilaya ya Babati ni Daraja jipya la Bacho iliyojengwa na Serikali kupitia wakala wa barabara Mjini na Vijijini (TARURA) kuimarisha mawasiliano katika Vijiji vitatu vya Haysam, Kiru NA Dareda.


Mingine ni ujenzi wa madarasa mapya matatu na Jengo la ofisi ya Walimu katika shule ya msingi Gidewar Kwa gharama ya Zaidi ya shilingi milioni 84.4. 


Baada ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Mwenge wa uhuru unaendelea na mbio zake katika halmashauri ya wilaya ya Hanang' kisha Mbulu na kuhitimishwa katika Mji wa Babati Oktoba 13 kisha kilele Oktoba 14 ikienda sambamba na kumbukizi ya kifo cha Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere na wiki ya vijana , Uwanja wa Kwaraa.  


#visionmediablog

#MwengeManyara 

#mwenge2023 

#Babati

BABATI DC YAPETA MIRADI YOTE, MWENGE WA UHURU 2023.  BABATI DC YAPETA MIRADI YOTE, MWENGE WA UHURU 2023. Reviewed by VISIONMEDIA on October 17, 2023 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.