Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Babati Mjini *Ndg Emmanuel Khambay* Oct 22,2023 ameongoza Harambee ya kuchangisha ujenzi wa kanisa la KKKT Sinai akiwa kama mgeni rasmi ambapo zilichangishwa *Milioni 72* na Ndugu. Khambay alichangia kiasi Cha *Tsh 3,600,000/= na Us dollar 200* na kufanya kiwango alichochangia kufika zaidi ya *milioni 4*
Sambamba na hayo *Ndg Khambay* alilitaka kanisa hilo kuendelea kuwafanya watu kuwa na *maadili mema* pamoja na *kulea watoto* kwa maadili mema ili kanisa lipate watu wa kulirithi huko Mbeleni. Pia ndugu Khambay, alishauri kanisa kupitia kwa Viongozi wao, kufungua *kituo cha daycare* ili watoto wa maeneo hayo wapate malezi bora na kuleta Viongozi bora wa baadaye.
*Mwisho*.Ndugu Khambay, aliwaomba Viongozi wa Kanisa hilo kuendelea kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan, pamoja na Viongozi wote wa Serikali kwa kazi zote wanazofanya kwa maslahi mapana ya Nchi
No comments: