test

Sabaya ajitia kitanzi Kiteto.

 SABAYA Isaskar (31) mkazi wa Njaniodo wilayani Kiteto mkoani Manyara, amekatisha uhai wake kwa kujinyonga kwa kutumia kamba aina ya manila, huku chanzo kikiwa bado hakijafahamika.




Kifo cha kijana huyo mwenye rika la Morani wa Kabila la Kimaasai kimevuta hisia kwa jamii huku ikielezwa kuwa kabila la kimaasai mtu kujinyonga huwa sio rahisi kwao.


Mwenyekiti wa Kijiji cha Partimbo aliyejulikana kwa jina la Kimirei amethibitisha tukio la kijana huyo ambapo amesema, "Toka tulivyopata taarifa kuwa hili tukio limetokea tulipata mshtuko lakini niwashukuru walioshiriki toka mwanzo marehemu alipoonekana maeneo yale ya tukio hadi kumfikisha hospitalini"




Sabaya ajitia kitanzi Kiteto. Sabaya ajitia kitanzi Kiteto. Reviewed by VISIONMEDIA on October 24, 2023 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.