Disemba 28, 2023 Bi Lovenes Hidana Mfanyabiashara wa Nguo za Watoto kutoka Moshi - Kilimanjaro amejishindia Milioni Tano katika Kampeni ya MAGIFTI DABO DABO kutoka Tigo inayoendelea hivi sasa.
Ikumbukwe Kampeni hii inayoendeshwa na Kampuni ya Tigo imezinduliwa wiki kadhaa zilizopita huku ikimtambulisha Haji Manara kama SEMAJI la Kampeni hii, ambapo mteja wa Tigo anaweza kushinda Fedha Taslimu hadi Milioni 10, Safari ya Kwenda Dubai au Zanzibar, Set ya Vifaa vya Ndani ambavyo ni Sound bar, Friji, TV na Microwave na Zawadi kubwa ya Magari Mawili ( 0km ) , kingine kinachovutia katika kampeni hii ni kwamba ukishinda kitu kimoja wapo kati ya ivyo unamchagua na yeyote umpendae ili apewe zawadi iyoiyo uliyoshinda hii ndio maana halisi ya MAGIFTI DABO DABO.
Akizungumza baada ya kumkabidhi Hundi ya Milioni 5 Mshindi , Meneja Mauzo wa Tigo Kilimanjaro Bwn.Silas Mkuyu amewasisitiza Wana Moshi na Watanzania kufanya miamala mbalimbali na Tigo Pesa kama Lipa kwa Simu, nunua vifurushi ili kuibuka washindi maana kampeni bado inaendelea
No comments: