✓ Tigo Tanzania Yazindua Promosheni ya "Soka la Afrika Limeitika" Itakayowapa Wateja Fursa ya Kuhudhuria Kombe la Mataifa ya Afrika 2024.
Meneja Huduma za Ziada Tigo, Adam Francis akimkabidhi mpira Mtaalam wa Huduma za Ziada Tigo, Noreen Kira, kuashiria uzinduzi wa promosheni ya Soka la Afrika Limeitika, ambapo watanzania 6 watashinda nafasi ya kwenda kutazama kombe la bara la Afrika ( AFCON 2024 ) nchini Ivory Coast , pamoja na Zawadi za Jezi na Fedha Taslimu hadi Milioni 10.Na Mwandishi Wetu.
Dar es Salaam, 28 Desemba 2023 – Tigo Tanzania, kampuni inayoongoza kwa mapinduzi ya KIDIGITALI Nchini Tanzania , inafuraha kutangaza uzinduzi wa promosheni yake mpya ya kusisimua inayojulikana kama , "Soka la Afrika Limeitika," inayowapa wateja fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali za Fedha Taslimu ikiwemo zawadi kubwa ya safari ya kushuhudia matukio ya kusisimua ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2024) yatakayofanyika nchini Ivory Coast.
Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika iliyopangwa kuanza Januari 13 hadi Februari 11, 2024, ina umuhimu wa kipekee kwa Tanzania, kwani timu ya taifa ya soka inafuzu kwa mara ya tatu katika historia ya michuano hiyo, ikiwa imeshiriki hapo awali 1980 na 2019.
Kama sehemu ya ofa, wateja sita waliobahatika watapata fursa ya kipekee ya kushinda safari yenye malipo kamili ili kufurahia mechi za moja kwa moja nchini Ivory Coast. Zaidi ya hayo, washindi watapata zawadi za jezi , mpira wa miguu, na zawadi za Fedha Taslimu hadi Millioni 10.
Ili kushiriki katika promosheni ya "Soka la Afrika Limeitika", unatakiwa kutuma neno "SOKA" kwenda 15670, ambapo utaulizwa maswali rahisi kuhusu SOKA ukijibu kwa usahihi ndivyo utajiongezea nafasi ya kushinda safari iliyolipiwa kwenda kushuhudia AFCON live nchini Ivory Coast , si hivyo tu bali pia washindi wengine wa Mipira , Jezi na Pesa Taslimu hadi Milioni 10 watapatikana .
Akizungumzia promosheni hiyo, Meneja wa Huduma Maalum Tigo, Adam Francis, alisema,“Tunafuraha kuzindua promosheni ya “Soka la Afrika Limeitika”, inayowapa wateja wetu wapendwa fursa ya kipekee ya kuwa sehemu ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2024. Promosheni hii sio tu inaendana na dhamira yetu ya kutoa uzoefu usio na kifani bali pia inasherehekea ushiriki wa Tanzania katika mashindano haya adhimu."
Tigo Tanzania inawahimiza wapenzi wote wa soka kujiunga na promosheni ya “Soka la Afrika Limeitika”, kusherehekea ari ya soka, na kupata nafasi ya kutengeneza kumbukumbu zisizosahaulika kwa kuhudhuria AFCON 2024.
Kwa maelezo zaidi kuhusu promosheni ya “Soka la Afrika Limeitika” na matoleo ya Tigo Tanzania, tafadhali tembelea Duka lolote la Tigo kote nchini au wasiliana na huduma kwa wateja wetu kwa nambari 100.
No comments: