Na Mwandishi Wetu.
Februari , 06 , 2024 Salim Ndaro Mfanya Biashara ndogondogo za kuuza matunda Mkoani Tanga anaenda kutimiza ndoto yake ya kujenga Nyumba bora na kuhama kwenye nyumba iliyochakaa aliyokuwa nayo baaada ya Kushinda Milioni 10 kutoka Tigo " MAGIFTI DABO DABO ".
Meneja Mauzo wa Tigo Kanda ya Pwani Abdul Amani Ally ( kulia ) akikabidhi Mfano wa Hundi kwa mshindi wa Milioni 10 za MAGIFTI DABO DABO Tanga , Salim Ndaro ( kushoto ) katika Hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwa Mshindi Mkoani Tanga.
Akizungumza baada ya kumkabidhi Hundi ya Milioni 10 Mshindi , Meneja wa Tigo Kanda ya Pwani Abdul Amani Ally amewasisitiza Wanatanga na Watanzania kufanya miamala kwa wingi na Tigo Pesa kama vile kununua LUKU , LIPA KWA SIMU , VIFURUSHI , KUTUMA NA KUPOKEA PESA , MALIPO YA SERIKALI n.k maana kuna zawadi kubwa ya Milioni hadi 30 na Magari Mawili yanaenda kutiolewa hivi karibuni.
Akizungumza kwa furaha kubwa, Mshindi wa Milioni 10 Bw. Salim amesema kwakweli haamini macho yake kama tukio lililokua linafanyika ni la kwelii,
" Mara ya kwanza napigiwa simu kuambiwa nimeshinda Milioni 10 ya MAGIFTI DABO DABO sikuamini kwakweli, Nilijua ni utapeli lakini baadae nkaja kuamini baada ya kuona kumbe nimepigiwa na namba 100 nawasihi Watanzania tumieni Tigo, fanyeni miamala maana ndo Siri ya Ushindi, mimi maisha yangu yanaenda kubadilika sasa naenda kujenga nyumba ya kisasa na kuhama kwenye hii nyumba iliyochakaa mnayoiona " alisemaSalim kwa furaha kubwa.
MKAZI WA TANGA ASHINDA MILIONI 10 YA TIGO , ATAJENGA NYUMBA
Reviewed by Adery Masta
on
February 06, 2024
Rating:
No comments: