Na Mwandishi Wetu.
Februari 09, 2024 Bi . Lilian Boniface Clement Mkazi wa Mwananyamala Jijini Dar Es Salaam anaenda kutimiza ndoto yake ya kufanya biashara kubwa ya uuzaji wa NAFAKA baada ya kushinda na kukabidhiwa rasmi Milioni 30 kutoka kampeni ya MAGIFTI DABO DABO inayoelekea Ukingoni.
Msemaji wa Kampeni ya Magifti Dabo Dabo HAJI MANARA akimkabidhi mfano wa Hundi ya Shilingi Milioni 30 Mshindi wa Promosheni ya MAGIFTI DABO DABO Lilian Clement Mkazi wa Mwananyamala Dar Es Salaam.
Ikumbukwe Kampeni hii inayoendeshwa na Kampuni ya Tigo ilizinduliwa wiki kadhaa zilizopita huku ikimtambulisha Haji Manara kama SEMAJI la Kampeni hii, ambapo mteja wa Tigo anaweza kushinda Fedha Taslimu hadi Milioni 10, Safari ya Kwenda Dubai au Zanzibar, Set ya Vifaa vya Ndani ambavyo ni Sound bar, Friji, TV na Microwave na Zawadi kubwa ya Magari Mawili ( 0km ) , kingine kinachovutia katika kampeni hii ni kwamba ukishinda kitu kimoja wapo kati ya ivyo unamchagua na yeyote umpendae ili apewe zawadi iyoiyo uliyoshinda hii ndio maana halisi ya MAGIFTI DABO DABO.
Akizungumza wakati wa tukio hilo Meneja wa Tigo Kanda ya Dar Es Salaam Bi. Beatrice Kinabo amewasisitiza wananchi wa Mwananyamala kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotangazwa na Kampuni ya Tigo ikiwemo utumiaji wa Tigopesa kwa wingi, ili kujishindia zawadi mbalimbali.
Akizungumza kwa furaha kubwa, Mshindi wa Milioni 30 Bi Lilian amesema kwakweli haamini macho yake kama tukio lililokua linafanyika ni la kwelii,
" Mara ya kwanza napigiwa simu kuambiwa nimeshinda Milioni 30 ya MAGIFTI DABO DABO sikuamini kwakweli, Nilijua ni utapeli lakini baadae nkaja kuamini baada ya kuona kumbe nimepigiwa na namba 100 nawasihi Watanzania tumieni Tigo, fanyeni miamala maana ndo Siri ya Ushindi, Pesa hii inaenda kubadilisha maisha yangu na kutimiza ndoto yangu ya kufanya biashara ya uuzaji na usambazaji wa nafaka.
HUYU HAPA MSHINDI WA MILIONI 30 KUTOKA TIGO
Reviewed by Adery Masta
on
February 09, 2024
Rating:
No comments: