test

TIGO KUTOA ZAWADI YA MAGARI MAWILI KWA WATEJA MWEZI HUU , SOMA HAPA

 


Washindi wakiwa mfano wa hundi ya pesa walizojishindia wapili kulia ni Ismail Rashid aliyejishindia vifaa vya Hisense na kushoto ni baba yake mdogo aliyemchagua kama mshindi mwenza ambaye naye anapatiwa seti yake ya vifaa hivyo.


Semaji la Magifti Dabodabo Haji Manara (kulia) akimpongeza Baba yake mdogo, Ismail Rashid aliyechaguliwa na mwanaye huyo kama mshindi mwenza wa zawadi ya vifaa vya Hisense (katikati) ni Ismail mwenyewe ambaye ndiye mshindi wa vifaa hivyo.

Na Mwandishi Wetu.

Monalisa Lazaro Kasonta , Hemed Swai ( Washindi wa Milioni Tano Tano ) , Eliva Eliazaro ( Mshindi wa Milioni Moja ) na Ismail Rashid Mshindi wa Vifaa vya Ndani kama vile TV , Friji, Sound bar na Microwave ambaye amemchagua Ba mdogo yake Idd Maulid kama Mshindi Mwenzake ni baadhi ya Washindi wachache wa MAGIFTI DABO DABO wiki hii.

Dar es Salaam, 2 Januari 2024: Kampuni ya mtandao wa simu ya Tigo kupitia kampeni yake ya Magifti Dabodabo leo imeendelea kuwanufaisha watumiaji wa mtandao huo kwa kuwapa zawadi zao washindi wanne waliopatikana wiki hii.

Neema hiyo wiki hii imewadondokea washindi wawili wa milioni tano kila mmoja, mshindi wa shilingi milioni moja na mshindi wa vifaa vya Hisense ambavyo ni seti ya friji, microwave, tv na redio ya muziki mnene (sound bar).

Ikiwa imebaki wiki Moja tu kuhitimishwa kwa Kampeni hii ya MAGIFTI DABO DABO Tigo inaendelea kutafuta Washindi zaidi wa Mamilioni ya Fedha Hadi Milioni 30 , Vifaa vya Hisense na Zawadi kubwa ya Magari Mawili ( 0km ) 

Kumbuka ili kuibuka mshindi wa Magari Mawili na Fedha Taslimu hadi Milioni 30 unachotakiwa ni kufanya miamala kwa wingi kupitia Tigo Pesa kama vile kununua vifurushi, Muda wa Maongezi, Bando, Malipo ya Serikali n.k Fanya hayo uibuke Mshindi nafasi bado ipoo

TIGO KUTOA ZAWADI YA MAGARI MAWILI KWA WATEJA MWEZI HUU , SOMA HAPA TIGO KUTOA ZAWADI YA MAGARI MAWILI KWA WATEJA MWEZI HUU , SOMA HAPA Reviewed by Adery Masta on February 02, 2024 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.