test

TIGO WATANGAZA KUTOA INTERNET BURE KILI HALF MARATHON 2024

 Na Mwandishi Wetu.

Februari 20 , 2024 Kampuni ya Mawasiliano nchini Tanzania Tigo, ambao pia ni Wadhamini wa Mbio za Kimataifa za Tigo Kili Half Marathon 21 Km, zitakazofanyika Jumapili ya Februari 25 , 2024 Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi , wametangaza kunogesha Mbio hizo kwa kutoa huduma mbalimbali za Kipekee kwa watakaohudhuria na Kushiriki. 

Akizungumza na waandishi wa Habari mapema Leo hii , Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini Bwn. Henry Kinabo amesema


" Tigo tutakuwa na Wi-Fi spots (Bure 4G) katika sehemu mbalimbali hapa mjini Moshi, Bar Amuz, Redstone, Moshi Pazuri, Kili Home pamoja na Moshi Club ambapo ndio Tamasha kubwa la Tigo Kili-Half International Marathon 2024 litafanyika. 

Kwa niaba ya Kampuni ya Tigo, naomba kuwaalika wageni wote mjini Moshi kujiunga nasi kwenye Kilimanjaro International Marathon hususani Tigo Kili- Half International Marathon " alimalizia Bwn Henry 


Ikumbukwe hadi sasa , nafasi kwa ajili ya kushiriki Mbio hizi Maarufu za 21Km tayari zimejaa ( SOLD OUT ) na zoezi la Kugawa Namba  lilianza Februari 17 - 18 Kwa upande wa Dar Es Salaam ,  na linaendelea Arusha Februari 20 - 21 Kisha Moshi  Februari 22 - 24 .

TIGO WATANGAZA KUTOA INTERNET BURE KILI HALF MARATHON 2024 TIGO WATANGAZA KUTOA INTERNET BURE KILI HALF MARATHON 2024 Reviewed by Adery Masta on February 20, 2024 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.