Naibu katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Tanzania bara Komredi Mussa Mwakitinya amesema Chadema waache kuweweseka kwani Chama cha Mapinduzi Kamwe hakijawahi kupoteza Ushawishi kwa Jamiii, ndugu Mwakitinya ameyasema hayo tarehe 28 Aprili 2p24 akizungumza na Maelfu ya Wananchi katika Mkutano wa hadhara katika Kishindo cha UVCCM kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 Mkoani Mtwara.
"Chadema waache kuweweseka na kujidanganya eti Chama cha Mapinduzi kimekosa Ushawishi kwa Jamii, Ndugu zangu CCM haijawahi kupoteza Mvuto kwa Jamii, ninyi mmeona ziara ya Katibu Mkuu wetu, namna chama kinavyokubalika huko mikoani, sasa kuna watu wanaongea mambo ya hovyo eti CCM Inakosa ushawishi kwa Jamii, hili haliko sawa na hatuwezi kulinyamazia"
"Kutokana na kazi kubwa inayofanya na Serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais wetu Dkt Samua Suluhu Hassan kusogeza huduma za kijamii karibu kama Maji, Umeme, Shule, na Hospitali Watanzania wanaendelea kukiamini Chama cha Mapinduzi sasa, kesho na mpaka kesho kutwa, ninyi mnaona maendeleo yanayofanyika nchi nzima. Hivyo hatutakosa ushawishi kwani tunafanya kile ambacho wananchi wanataka"
Aidha Ndugu Mwakitinya ameonyesha kukerwa na baadhi ya Viongozi wa Chadema wanaosema wanachukizwa na kitendo cha Wana CCM kumsifu na Kumpongeza Rais Samia kwa kazi Kubwa anayoifanya ya kuwatumikia Watanzania
"Ndugu zangu kuna watu hawa hovyo sijui wanakereka nini tukimsifu na kumpongeza Mwenyekiti wetu na Rais wa Jamahuri ya Muungamo wa Tanzania kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya, Sawa Serikali ndio inatoa pesa lakini anayeridhia michakato na kuruhusu pesa zikafanye jambo fulani ni Rais Samia, na hili halijaanza leo kwani tumekua na utamaduni wetu wa kuwapongeza Viongozi wetu kwenye kila awamu kwa kazi zao"
"Tunampongeza Rais Samia kutokana na kazi kubwa anayoifanya ya kuleta maendeleo kwa Watanzania na hili hatutaliacha tutaendelea kumtia Moyo ili azidi kuteletea maendele ili nyie mnokereka na maendeleo mzidi kukereka lakini wananchi wafurahie maendeleo yao.
"Watanzania msikubali kujazwa Chuki kuna chama chenyewe kimeamua kufanya Maandamano lakini kwenye Maandamano yao haya ambayo hayana kichwa wala miguu kazi zao ni kujaza chuki kwa wananchi dhidi ya serikali
"Siku kadhaa zilizopita kiongozi mkuu wa Chama hicho alisema kuna wakati utafika kama noma na iwe noma! Kaili hizi kauli ni kauli za hovyo na za kichochezi zinapaswa kupingwa kwa hali ya juu kwani mtu kama huyu dhamira yake ni kutaka kumwaga Damu ya Watanzania".
No comments: