test

WALIPENI WAFANYAKAZI VIZURI,MD MATI SUPER BRAND'S LTD.

 Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Mati super Brand's iliyopo mkoani Manyara bwana David Mulokozi amewataka waajiri wenzake wa makampuni binafsi mkoani humo kuwalipa watumishi wao stahiki zao ikiwemo mishahara kwa wakati pamoja na kuwapa mikataba ya ajira.


Mulokozi ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani MEI MOSI ambayo kimkoa imeadhimishwa Machi 29,2024 katika viwanja vya Tanzanite Kwaraa mjini Babati mkoani Manyara.
Amebainisha kuwa ili makampuni yaweze kufanya vizuri na kukua kiuchumi ni lazima waajiri wawajali wafanyakazi wao wanaofanya kazi za uzalishaji katika kampuni kwa kuwalipa vizuri stahiki zao pindi wawapo kazini.
Wafanyakazi wa kampuni ya Mati super Brand'inayojihusisha na uzalishaji wa vinywaji changamshi Kama vile,Sed Pineapple, Strong drygin,Tai, Tanzanite premium Vodica n.k wakiwa katika picha ya maandamano kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani MEI MOSI ambayo kimkoa imeadhimishwa Machi 29 Mkoani Manyara. 
#vision media tz 
WALIPENI WAFANYAKAZI VIZURI,MD MATI SUPER BRAND'S LTD. WALIPENI WAFANYAKAZI VIZURI,MD MATI SUPER BRAND'S LTD. Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on April 29, 2024 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.