Mgeni rasmi katika kilele cha Maadhimisho ya Kimataifa ya Usalama na Afya mahala pa kazi , Naibu Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Doto Biteko akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Afya na Usalama mahala pa Kazi wa Kampuni ya Tigo Bwn. Dismas Anthony , kuhusu namna Tigo inavyoshirikiana bega kwa bega na serikali katika kuhakikisha usalama wa wafanyakazi kuwa ni jambo linalopewa kipaumbele , kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Kazi , Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi.
Na Mwandishi Wetu .
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dotto Biteko Leo, Aprili 28 , 2024 ametembelea Banda la Kampuni ya Tigo kwa lengo la kujionea huduma mbalimbali za kidigitali zinazotolewa na kampuni hiyo katika kilele cha Maadhimisho ya Kimataifa ya Usalama na Afya mahala pa kazi viwanja vya General Tyre Jijini Arusha.
Ikumbukwe Kampuni ya Tigo kama ilivyo miaka yote , imeshiriki katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Usalama na Afya Mahala pa kazi tangu Tarehe 23 , April hadi leo Tarehe 1, Mei 2024 yalipohitimishwa.
NAIBU WAZIRI MKUU ATEMBELEA BANDA LA TIGO , KILELE CHA MAADHIMISHO YA USALAMA NA AFYA KAZINI
Reviewed by Adery Masta
on
April 28, 2024
Rating:
No comments: