test

TIGO WAMWAGA SIMU ZA MKOPO WIKI YA USALAMA NA AFYA MAHALA PA KAZI 2024

 

Meneja Mauzo wa Tigo Mkoa wa Arusha, Ryami Fatala akimkabidhi simu mkaazi wa Arusha, John Mtaka,katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Usalama na Afya mahala pa kazi , yanayoendelea Jijini Arusha.

Na Mwandishi Wetu.

Kampuni ya Tigo kama ilivyo miaka yote , inashiriki katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Usalama na Afya Mahala pa kazi yanayoendelea Jijini Arusha tangu Tarehe 23 , April na Kilele chake kitakua Tarehe 1, Mei mwaka huu 2024.

Akizungumza na Mwandishi wetu katika Banda la Tigo lililopo katika Maadhimisho hayo , Mfanyakazi wa Tigo katika Kitengo cha Usalama na Afya Kazini Bwn. Dismas Antony amesema Tigo kama mdau mkuwa wa OSHA ambao ni waandaaji wa Maadhimisho haya imekua ikishiriki kwa Takribani kila mwaka na katika Maadhimisho haya yenye kauli Mbiu " Athari za Mabadiliko ya Tabia ya Nchi katika Usalama na Afya Mahala pa kazi "

" Tigo kama kampuni tunahakikisha tunawalinda wafanyakazi wetu , lakini katika Maonesho haya tuna zawadi nyingi kwa wateja wetu huduma zote za Tigo zipo hapa ikiwemo simu za Mkopo"

TIGO WAMWAGA SIMU ZA MKOPO WIKI YA USALAMA NA AFYA MAHALA PA KAZI 2024 TIGO WAMWAGA SIMU ZA MKOPO WIKI YA USALAMA NA AFYA MAHALA PA KAZI 2024 Reviewed by Adery Masta on April 26, 2024 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.