Katibu mkuu jumuiya ya wazazi wa ccm Taifa Ally Hapi mei,10/2024 ameitikisa Manispaa ya Singida baada ya maelefu ya wananchi wa manispaa hiyo kujitokeza kumlaki na kumsikiliza katika mkutano mkubwa uliofanyika katika viwanja vya standi ya zamani ambapo historia imendikwa hii ni kutokana na wananchi kuelewa kazi inayofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea maendeleo.
Akiwa manispaa ya singida hapi amefanya shughuli mbalimbali ikiwemo kutembela na kuzungumza na wanachama wa chama cha mapinduzi ccm katika ngazi ya mashina ambapo katika mikutano hiyo ameeleza namna chama hicho kinavyotambua mchango wa viongozi katika ngazi ya matawi, mashina na mabalozi kwani ndiyo wenye wati katika maeneo yao.
"Mwenyekiti wetu wa chama cha mapinduzi na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan anathamini sana kazi mnayoifanya viongozi wa ngazi zote na anawawazia mema,sote tunajua kazi kubwa mnayoifanya ndiyo maana nimekuja kuwaona na kuongea nanyi hivyo msijisikie wanyonge chama Taifa tupo pamoja nanyi,ninyi ndiyo ushindi wa ccm katika chaguzi zote zijazo kama mnavuofahamu mwaka huu tuna uchaguzi na mwakani pia ushindi wa chama chetu unatokana na kazi yenu nzuri mnayoifanya"alisme akiwa katika shina namba 2 tawi la Majengo kata ya majengo na shina la Kasimu Majaliwa tawi misuna kata ya misuna kabla ya kuelekea katika mkutano
Akiwa katika mkutano wa Hadhara katika viwanja vya stendi ya zamani Katibu mkuu huyo amezungumza na wananchi huku akigusia masuala kadhaa ya maendeleo akieleza dhamira ya serikali na chama ya kuwaletea maendeleo ambapo Hapi amewahakikishia wananchi kuwa chama cha mapinduzi kitaendelea kuisimamia serikali katika utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020/25 katika sekta zote.
"Tunajua yapo mengi serikali imefanya na imetekeleza ikiwa ni katika utekelezaji wa ilani ya chama chetu ambayo tuliinadi kwenu mwaka 2020 wajibu wetu kama chama kama jumuiya ya wazazi ni kuisimamia serikali iendelee kutekeleza miradi ya maendeleo na kutatua kero za wananchi ndiyo maana kila mkutano wangu ninawahimiza watumishi wa umma kutekeleza kufanya kazi zao kwa weledi na kutumia muda wao kutatua kero za wananchi,nimewataka na kuwaelekeza watoke ofisini kwenda kutatua kero kuhamasisha maendeleo katika maeneo ya wananchi hii ndiyo nguzo kubwa ya kuunga mkono kazi inayofanywa na Rais wetu"alisema hapi
Kuhusu kazi zinazofanywa na serikali Hapi amewataka wananchi kuendelea kumuunga mkono kiongozi mkuu wa nchi kwa maono makubwa aliyo nayo ya kuwatumikia wananchi kwani ameendelea kutoa fedha kwaajilinya utekelezaji wa miradi katika sekta ya afya hospitali nyinyi zimejengwa,vituo vya afya vimejengwa,zahanati kila kijiji lengo ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya katika maeneo yao,pia katika sekta ya maji Rais ametoa fedha nyingi kwaajili ya utekelezaji wa miradi ya maji,kwenye umeme kila kijiji kimepata umeme,miradi ya barabara huko ndiyo usiseme na maeneo mengine mengi.
"Wakati Rais samia anaingia madarakani aliikuta miradi ya kimkakati ikiwa imeanza tu utekelezaji mfano mradi wa bwawa la mwalimu Nyerere alikuta upo asilimia 34% pekee lakini leo umefikia zaidi ya asilimia 90% na umeme umeunganishwa katika njia kuu ya Taifa(grid ya taifa) mradi wa reli ya umeme leo tunapozunguma mradi umefika mbali na miradi mingine,niwaombe ndugu zangu hakuna wakati mwingine wa kumuunga mkono Rais wetu kama wakati huu anatupenda sana watanzania"alisema hapi
No comments: