test

Kizimbani, Kwakuzini na Mwanae.

 



Mkazi wa Nyakato mkoani Mwanza, Bashiri Mohamed (35), amefikishwa mahakamani leo Mei 21,2024, na kusomewa shtaka moja la kuzini na maharimu.



Mshtakiwa huyo amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza na kusomewa shtaka hilo lenye kosa analodaiwa kulitenda kati ya Septemba hadi Februari 15, 2024.


Akisoma shtaka hilo, mwendesha mashtaka wa serikali Mwanahawa Changale amesema; "Mshtakiwa kwa tarehe tofauti kuanzia Septemba 2023 hadi Februari 15, 2024, eneo la Nyakato-Mecco, wilaya ya Ilemela anadaiwa kuzini na maharimu (16) huku akitambua ni mtoto wake wa kumzaa."


Amesema mshtakiwa ametenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 158 (1) (a) cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai sura ya 16  marejeo ya mwaka 2022.


Hata hivyo, baada ya kusomewa shtaka hilo, mshtakiwa amekana shtaka na kuomba apatiwe dhamana.


Baada ya maelezo hayo, Hakimu Mkazi Mwandamizi, wa mahakama hiyo Juma Opudo amemtaka mshtakiwa kutimiza masharti ya dhamana ambayo ni kuwa na wadhamini wawili watakosaini hundi ya maneno ya Sh 4 milioni kila mmoja na mwingine awe na mali isiyohamishika.


Hata hivyo, mshtakiwa amekwama kutimiza masharti ya dhamana kwani barua ya udhamini ya mdhamini mmoja aliyetokea wilayani Magu haikuthibitishwa na Hakimu Mfawidhi wa wilaya yake.


"Barua yako sitoipitisha kwa sababu unatokea wilaya nyingine na haijapita kwa Hakimu Mfawidhi wa wilaya unayotoka. Shauri litaitwa kesho kwa ajili ya kutajwa ili kukamilisha mchakato wa dhamana," amesema.


Hakimu ameahirisha Shauri hilo hadi Juni 11, mwaka huu litakapoitwa kwa ajili ya mshtakiwa kuanza kusomewa hoja za awali.



Kizimbani, Kwakuzini na Mwanae. Kizimbani, Kwakuzini na Mwanae. Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on May 21, 2024 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.