MANYARA.
Madiwani katika halimashauri ya wilaya ya Babati mkoani Manyara wametakiwa kuhakikisha wanasimamia wanafunzi katika zao wanapata chakula cha mchana pindi wawapo shuleni.
Hayo yameelezwa na mwenyekiti wa halimashauri ya wilaya ya Babati bw.John Noya wakati akizungumza kwenye Baraza la robo ya tatu la madiwani wa halimashauri hiyo lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halimashauri ya wilaya ya Babati.
Amesema kumekuwepo na kulegalega kwa baadhi ya shule zilizopo katika kata za Babati vijijini kwa kutowapati chakula wanafunzi Jambo ambalo halikubaliki kwani ni lazima wanafunzi wote wapate chakula cha mchana pindi wawapo shuleni kwani ni hali yao ya msingi.
Kwa upande katibu tawala wa halimashauri ya wilaya ya Babati bw.Halphan Mtipula akizungumza katika Baraza hilo amewasisitiza madiwani kutilia mkazo suala hilo kwani jambo hilo la chakula mashuleni ni agizo kutoka serikalini hivyo ni lazima litekelezwa
No comments: