SUPHIAN APANDA MITI 1000 PUMA SEKONDARI ALIPOSOMEA, SINGIDA MPYA YA KIJANI INAWEZEKANA YAZIDI KUNOGA
.
Mdau wa Mazingira nchini na kada machachari wa CCM, Suphian Juma Nkuwi leo amepanda miti 1000 Shule ya Sekondari Puma mkoani Singida aliposomea kama sehemu ya kurudisha fadhila shuleni hapo.
Akizungumza na wanafunzi wa Shule hiyo, ndugu Nkuwi amewaambiwa wanafunzi wa Shule hiyo yenye wanafunzi 1000 kwamba wakati anasoma hapo miaka ya 2000 alikuwa anashika namba moja darasani kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne kwasababu alitunza mazingira na miti ndiyo afya ya akili.
"Miti hutupatia sisi binadamu oxygen ambayo ndio hufanya akili na mwili kufanya kazi vizuri, itunzeni, nyie ndio baba na mama wa miti hii, mimi ilinifanya nikawa ana akili na nikafaulu vema darasani na kushika namba moja kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne."
Aidha Mgeni rasmi wa kampeni hiyo iliyozinduliwa Aprili 14, 2024 ikimuunga mkono Rais Dkt Samia kwenye uthibiti dhidi ya mabadiliko ya Tabia nchi, inayofadhiliwa na Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS), Askari Mhifadhi Tresia Gabriel Kasigara amewataka wanafunzi kutomwangusha ndugu Suphian kwa kutoitunza miti hiyo ya kivuli na matunda kwani bila miti hakuna nyuki, na bila nyuki hakuna maisha ya binadamu.
Kwa upande wa shukrani za Shule, Mkuu wa Shule ya Sekondari Puma, ndugu Hussein Malonga amempongeza Suphian kwa kuleta zawadi ya miti huku akiwaambia wanafunzi waige tabia yake, na pia kuwaagiza kila mwanafunzi kutunza miti wake hadi atakapohitimu Shule na kuhakikisha unakua vizuri.
Ndugu Suphian amehitimisha hotuba yake kwa kuwaomba wadau mbali mbali nchini na nje ya nchi kujitokeza kuifadhili kampeni hiyo ili kutimiza lengo lake la Kupanda miti milioni moja kupunguza athari za kimazingira na kuurejesha mkoa wa Singida kwenye uoto wake wa asili uliopotea kutokana na shughuli za kibinadamu.
No comments: