SOKO LA KATESH BAADA YA MAFURIKO RC Sendiga aagiza shughuli katika soko la Katesh kuanza mara moja kabla ya Mei 24
Mhe. Mkuu wa mkoa wa Manyara amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang Ndg. Ibrahim Mbogo na viongozi wa soko jipya la Katesh kufanya uhakiki wa wafanyabiashara pamoja na kukaa kikao na wafanyabiashara wa soko hilo.
Mhe. Queen Cuthbert Sendiga ameyasema hayo leo Mei 16, 2024 alipofanya ziara katika soko jipya la Katesh lililopo katika Wilayani Hanang.
RC Sendiga amesema kuwa lengo la kukaa na wafanyabiashara hao ni pamoja na kuwapa taratibu za soko hilo na kutatua changamoto zilizopo kabla wafanyabiasha hawo kuhamia na kuanza kufanya shughuli zao katika soko hilo jipya kutoka soko walilokua awali.
Aidha, Mhe. Sendiga ameagiza shughuli katika soko hilo kuanza mara moja kabla ya siku ya Ijumaa Mei 24, 2024 ili kutoa huduma kwa Wananchi na kuchochea uchumi wa wafanyabiashara.
SOKO LA KATESH BAADA YA MAFURIKO RC Sendiga aagiza shughuli katika soko la Katesh kuanza mara moja kabla ya Mei 24
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
May 16, 2024
Rating:
No comments: