Askari Polisi nchini wametakiwa kuzingatia maadili wanapotekeleza majukumu yao huku suala la nidhamu likisisitizwa kuwa kipaumbele.
Wito huo umetolewa leo Mei 22,2024 na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, CP Awadhi Juma Haji alipofanya ziara ya kikazi mkoani Mwanza.
Akizungumza na Maafisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali CP Awadhi ametaja mambo manne yanayotakiwa kuzingatiwa na Polisi kuwa ni nidhamu, haki, weledi na uadilifu.
"Ninapenda nitumie kikao hiki kusema suala la ukiukwaji wa maadili lina "zero tolerance" hatuna mzaha wala huruma kwenye suala la nidhamu " amesema CP Awadhi.
Aidha, amekagua vikosi vya Polisi ikiwemo, Usalama barabarani, Mbwa na Farasi na Kikosi cha Kutuliza Ghasia lakini pia alikagua vikundi vya CRT na kutoa maelekezo yatakayoimarisha weledi katika shughuli zao.
Lengo la ukaguzi huo ni kutathimini hali ya utayari kwa maafisa wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbi kuelekea uchaguzi wa serikali za mtaa oktoba 2024 na baadaye uchaguzi mkuu 2025.
Mbali na kupongeza jitihada zinazofanywa na Askari Polisi mkoa wa Mwanza kwa kuendelea kufanya mkoa kuwa salama, pia amewapongeza Maafisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali waliopandishwa vyeo hivi karibuni kutokana na utendaji kazi wao mzuri.
Baada ya ukaguzi huo CP Awadhi ametembelea eneo la bandari ya Mwanza Kaskazini na kujionea shughuli ya unasuaji wa meli ya MV Clarias iliyoegemea upande mmoja majini unavyoendelea.
UTAYARI, kuelekea Uchaguzi, Askari wahimizwa kuzingatia maadili
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
May 23, 2024
Rating:
No comments: