Watu watatu waliojifanya Wafanyabiashara wa Madini wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Manyara wakituhumiwa kumtapeli Mfanyabiashara wa madini zaidi ya Sh. Mil 49.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo SACP. George Katabazi amesema pesa hizo pamoja na gari lenye namba za usajili T 146 DGS aina ya RAV 4 zilichukuliwa kwa mfanyabiashara huyo wa Mkoani Kilimanjaro na kusema Watuhuniwa hao walikiri kuzipata fedha hizo kwa njia ya utapeli.
Amesema, “ Kuna baadhi ya wananchi hawajitumi katika kufanya kazi na badala yake wamekuwa wakijitafutia fedha kwa njia zisizo halali na kijikuta wanaingia hatiani, tumewakamata watuhumiwa hao majira ya saa kumi na mbili jioni, tuliwahoji kwa kina na kuwapekua na wakakiri ni kweli wamejipatia fedha hizo kwa njia ya utapeli.”
Kamanda Katabazi amesema majina ya watuhumiwa yamehifadhiwa na kwamba mara baada ya uchunguzi watuhumiwa watafikishwa Mahakamani ili Sheria ifuate huku akitoa wito kwa Wananchi kuacha tabia ya kuwaamini watu wasiowafahamu, ili kuondokana na madhara yatakayojitokeza.
No comments: