test

Sugu Amburuza Mch Msigwa Uenyekiti CHADEMA Nyasa.

 Mbunge wa zamani wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu ametangazwa mshindi kwenye uchaguzi wa kumtafuta Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kanda ya Nyasa na kumuwangusha aliyekuwa anatetea kiti hicho, Mchungaji Peter Msigwa.



Matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika leo Mei 29, 2024 katika Mji wa Makambako Mkoani Njombe yametangazwa usiku huu baada ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema Kanda ya Nyasa kupiga kura.


Sugu ameshinda kwa asilimia 51 huku Mchungaji Msigwa akipata asilimia 49 ya kura zilizopigwa.


Kwa upande wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Mshindi ni Frank Mwakajoka ambaye ni Mbunge wa zamani wa Tunduma.

Sugu Amburuza Mch Msigwa Uenyekiti CHADEMA Nyasa. Sugu Amburuza Mch Msigwa Uenyekiti CHADEMA Nyasa. Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on May 29, 2024 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.