test

BIHIMBA ATOA LAKI TANO UJENZI WA MSIKITI

  Na Mwandishi Wetu.

Mwanaharakati huru Bihimba Nassoro Mpaya leo Juni 17,2024 ametoa jumla ya Shilingi Laki tano (5) kwaajili ya kununua Matofali 500 ambayo yatatumika katika ujenzi wa Msikiti unatarajia kuingia Waumini wa Dini ya Kiislam 200 huko Kigezi Machimbo (Chanika) Wilaya ya Ilala Jijini Dar es salaam. 

Akizungumza wakati akikabidhi fedha hizo Bihimba amesema kuwa hapo awali alitoa Matofali 1750 na Mifuko Kumi (10) ya Simenti na leo ametoa Matofali Mia tano (500 ) hivyo mpaka sasa  jumla ya Matofali yote ni 2250.


 
Pamoja na hayo Ustadhi Amiri Musa Mohammed wa Madrasa ya Ally & Rahma Alhinai  amemshukuru Mwanaharakati huyu kwa kujitoa  tangu kuanza kwa ujenzi wa Madrasa mpaka sasa wanapotarajia kujenga Msikiti . 

Aidha Bihimba amehaidi kujitoa zaidi na zaidi katika kulifanikisha hilo.

BIHIMBA ATOA LAKI TANO UJENZI WA MSIKITI BIHIMBA ATOA LAKI TANO UJENZI WA MSIKITI Reviewed by Adery Masta on June 17, 2024 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.