Aida Juma Mkina Mkazi wa Dar es Salaam ( Katikati ) ambaye ni mshindi wa tiketi ( Wiki ya Tatu ) Kampeni ya ZIGO la EURO CUP na Hisense, safari iliyolipiwa kila kitu kwenda kutazama mechi za Kombe la Euro moja kwa moja nchini Ujerumani kuanzia hatua ya 16 bora, akikabidhiwa Mfano wa Tiketi tukio lililofanyika mapema leo hii June , 14 , 2024 Makao makuu ya Tigo Jijini Dar Es Salaam , Bi. Aida ameibuka mshindi baada ya kubashiri Mechi na PariMatch kupitia Tigo Pesa Super App, Kushoto ni Meneja wa Wateja Maalum Tigo Pesa Bi. Mary Ruta akifuatiwa na Balozi wa Kampeni hii " MWAISA " na kulia ni Mwakilishi kutoka Hisense.
Na Adery Masta.
Aida Juma Mkazi wa Dar Es Salaam, ni Mteja wa Tigo wa tatu kujishindia Safari iliyolipiwa kila kitu ya kwenda kutazama Mechi za Kombe la EURO 2024 , ambapo timu 24 zinatarajiwa kuchuana katika miji 10 mwenyeji Nchini Ujerumani .
Aida ameshinda kupitia Kampeni ya ZIGO LA EURO CUP NA Hisense , iliyozinduliwa wiki kadhaa Zilizopita ambapo Kampuni ya Mawasiliano ya TIGO, kwa kushirikiana na Parimatch na Hisense waliileta kusambaza Tabasamu kwa Wateja wao , Ikumbukwe Aida ni Mshindi wa Wiki ya Tatu akitanguliwa na Ramadhan Mrutu Mshindi wa Wiki ya Kwanza na Emmanuel Mlonjela Mshindi wa Wiki ya Pili , huku katika wiki hii ya Tatu Washindi Wengine kama Habibu Mkazi wa Bagamoyo amejishindia Friji na TV ya Hisense , Faridi Hashim na wengine kibao wakijishindia Pesa Taslim Milioni Moja Moja.
Ili kuingia kwenye droo na kupata nafasi ya kujishindia tiketi au zawadi ya fedha taslimu TZS 1,000,000, na Vifaa vya Hisense TV na Friji washiriki wanapaswa kujiandikisha na Parimatch, kuweka pesa zao kupitia Tigo Pesa kisha kuweka dau ( betting ) kwenye mechi yoyote ya mpira wa miguu na Parimatch. Kadiri dau zinavyowekwa, ndivyo nafasi zinavyoongezeka ya kushinda TZS 1,000,000 au tiketi ya safari na mechi yenye malipo kamili ya kwenda kutazama mechi za Kombe la Euro moja kwa moja nchini Ujerumani kuanzia hatua ya 16 bora.
Akizungumza Wakati wa Kugawa zawadi kwa Washindi , Meneja wa Wateja Maalum Tigo Pesa Bi. Mary Ruta amesema
" Ndo kwanza ni droo ya tatu ya Kampeni yetu ya ZIGO LA EURO na Hisense , kama ambavyo inajulikana Kampeni hii tunatafuta Washindi wa Tiketi ya Kwenda kushuhudia Mechi za Euro ambalo Mechi tayari zimeanza rasmi , Washindi wa Vifaa vya Hisense ambavyo ni Friji na Tv ya Kisasa , na Washindi wa Pesa Taslimu.
Zawadi bado zipo nyingi kwa maana Leo ndo Washindi wa Droo ya tatu, bado Kuna Droo nyingine nyingi zinawasubiri , Tumia kwa wingi TIGO Pesa Super App , Bashiri na Parimatch kupia App ya Tigo Pesa ili kutengeneza mazingira ya kujishindia zawadi za Tv na Friji kutoka Hisense , Fedha Taslimu Hadi Milioni Moja na Zawadi kubwa ya kwenda kushuhudia Mechi za EURO CUP 2024 " alimalizia Mary Ruta
KAMA UTANI : MREMBO BINGWA WA KUBASHIRI NA PARIMATCH APELEKWA UJERUMANI KUSHUHUDIA EURO
Reviewed by Adery Masta
on
June 15, 2024
Rating:
No comments: