Aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama cha ADC Doyo Hassani Doyo anatarajia kuchukua fomu ya kugombea uenyekiti Taifa June 11 mwaka huu.
Doyo anakwenda kumrithi Mwenyekiti Taifa Hamad Rashid aliyemaliza muda wake kikatiba.
Amesema lengo kuu la kugombea nafasi hiyo kuwa ni kuleta mabadiliko ya sheria ,Hali ya ajira na maisha Bora kwa kila mtanzania lakini pia nimekomaa kisiasa.
Amesema Kipekree nimshukuru Mwenyekiti wa chama Taifa Hamad Rashid Mohamed kwa kuonyesha ukomavu wa kisiasa kwa sababu amenifundisha siasa kwa kipindi cha miaka kumi.
Amesema viongozi wengi wanapenda kunga'ng'ania madaraka lakini kwa Mwenyekiti wetu ni tofauti ni mwanasiasa aliyeonesha mfano wa kuigwa kwa watanzania.
"Ifike hatua nafasi unayopewa na wenzako lazima ufate katiba ya nchi nina imani wanasiasa wengine watafuata nyayo za Hamadi Rashid ili kuacha wanachama wapya ili kuweza kufanya kazi",amesema Doyo.
Aidha amemkaribisha msingwa kuhamia chama cha ADC kwa lengo la kuongeza nguvu ili kiwe chama cha ushindani.
Amesema June 20 nina safari ya kuzunguka ili kutafuta wadhamini watakaonidhamini ili niweke kushinda ni lazima ni pate wadhamini wasiopunguwa 150 ,75 kutoka Zanzibar na 75 kutoka Tanzania Bara.
Amesema nimefurahi kwamba uongozi wa chama umenipa baraka katika nafasi yangu niliyotangaza .
Sababu kubwa ni kwamba tayari nimejifunza vitu vingi kutoka kwa Hamadi Rashid nimefanya nae kazi kwa kipindi cha miaka 10 mfululizo .
Nawahakikishia watanzania na kuwatoa hofu wananchi na watanzania wote ahadi yangu ni kwamba tunakwenda kukiimarisha chama kwa ngazi ya juuu.
No comments: