Na Adery Masta.
Benki ya Equity inajivunia kuendelea kuwa na mikakati thabiti kwa ajili ya wakulima Nchini kwa kutoa mikopo mbalimbali kama vile pembejeo , Trekta na Mitaji ambapo tangu mwaka uanze benki iyo imeweza kutoa mikopo ya Shilingi Bilioni 46 ikiwa ni katika mazao ya mahindi , pamba , Alzeti n.k
Hayo yamebainishwa Leo Julai , 02 , 2024 na Meneja Mkuu wa Biashara - Equity Bank Bi. Leah Ayoub wakati akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa Banda lao jipya kabisa katika Maonesho ya 48 ya Biashara Kimataifa Sabasaba , lililoko Maonesho Avenue Viwanjani humo .Aidha Bi. Leah amesema Equity Bank imejipanga kisawasawa kuwahudumia wateja watakao tembelea banda lao katika maonesho hayo
" Tunawakaribisha sana wateja wetu , msimu huu wa sabasaba tuna ofa mbalimbali kwa ajili ya wateja wetu wadogo na wakubwa Huduma kama kutoa na kuweka fedha , Mikopo midogo na mikubwa , Huduma ya Benki Kidigitali kupitia HAPO HAPO AKAUNTI rahisi kabisa kwa kupiga *150*07# , Simu yako Benki yako popote ulipo utapata huduma za EQUITY Benki ikiwemo kufungua akaunti " amesema Aidha amewasisitiza wakulima kuchangamkia fursa hii ya Mikopo na huduma nyingine kibao za benki iyo hasa msimu huu wa sabasaba.
EQUITY BANK WAJA KIVINGINE SABASABA
Reviewed by Adery Masta
on
July 02, 2024
Rating:
No comments: