Na Adery Masta.
Agosti , 27 , 2024 Kampuni namba moja nchini kwa utoaji wa Huduma za Kidigitali Tigo Tanzania kwa kushirikiana na ZMOTION SOLUTIONS, wameendesha mafunzo ya siku moja kwa wamiliki na wakurugenzi wa shule binafsi kuhusu huduma ya LIPA ADA.
Ikumbukwe Huduma hii ya LIPA ADA ilizinduliwa miezi kadhaa iliyopita na inarahisisha Kulipa na kupokea Ada na Tigo Pesa , Wateja wa Tigo Pesa wanaweza kupiga *150*01#, kisha bonyeza 4 kwa Malipo ya Bili, 2 kwa Kutafuta Kampuni, 9 kwa UTT AMIS & Elimu, 4 kwa Lipa Ada, na kisha ingiza namba ya shule na fuata maelekezo. Vinginevyo, wanaweza pia kulipa kupitia mawakala wa Tigo Pesa waliopo nchi nzima
Mafunzo hayo yamefanyika , yakiwa na lengo la kuhakikisha ufanisi wa mfumo huo mpya ambao unatoa fursa kwa wazazi kulipia ada kidogo kidogo kulingana na uwezo wao.
Mkurugenzi wa Biashara-Tigo Pesa, Bw. James Sumari, alieleza kuwa mfumo wa ‘LIPA ADA’ ni mojawapo ya ubunifu wa kiteknolojia uliolenga kutatua changamoto zinazowakumba wazazi na shule katika suala la ulipaji ada. Aliongeza kuwa malipo kupitia mfumo huu yatakuwa yakifanyika kupitia huduma ya TigoPesa, hivyo kurahisisha mchakato mzima .
Bw. James ameongezea kuwa Tigo Pesa ina mpango wa kupeleka fursa hii hata mikoani ili kuwafikia wamiliki wa shule wengi zaidi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa ZMotion Said Ally alibainisha kuwa mfumo wa ‘LIPA ADA’ umesanifiwa kwa kuzingatia mahitaji ya shule binafsi na ni rahisi kutumia
No comments: