Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde amekabidhi zawadi za pikipiki, simu janja za mkononi pamoja na baiskeli kwa washindi promosheni ya vuna na tigo pesa iliyofanyika hivi karibuni jijini Dodoma.
Silinde amekabidhi zawadi hizo wakati wa ufunguzi wa uzinduzi wa Maonesho ya Samia Kilimo Biashara expo
Kwa upande wake Mkurugenzi wa tigo pesa Kanda ya mashariki inayohusisha mikoa ya Tanga na morogoro Bw Abdul Ally ambaye amesema huu ni muendelezo wa kampuni hiyo kutoa ZAWADI kwa wateja wao hususani kupitia droo za mara kwa mara zinazotolea na kampuni hiyo.
Wakizungumza mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao washindi wa shindano Hilo, (Said Dole) wamewataka wakulima wengine kuendelea kutumia huduma ya Tigo pesa kwani ndio salama na rahisi ukilinganisha na mitandao mingine.
Kampuni ya Tigo Tanzania imeendelea kutoa huduma hapa nchini kwa Zaidi ya miaka 30 sasa ambapo mapema wiki hii ilizindua kampeni maalum ya wiki ya huduma kwa mteja iliyoenda sambamba ushirikiano WA kibiashara na Shirikisho la Relief Tanzania (TRC).
No comments: