test

JELA MAISHA KWA KUBAKA MTOTO WA MIAKA 8

Samwel Anthony (34) mkazi wa kijiji cha Shilima amehukumiwa na mahakama ya wilaya ya Kwimba kifungo cha maisha jela kwa kubaka mtoto wa miaka 8.

Hukumu hiyo imetolewa leo tarehe 20.11.2024 na hakimu mkazi mkuu Ndeko Dastan Ndeko ambaye ndio hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo baada ya kusikiliza mashahidi 5 wa Jamhuri akiwemo mhanga, mahakama imejiridhisha pasi na kuacha shaka kwamba mtuhumiwa ametenda kosa hilo.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka iliyosomwa na mwendesha mashtaka wa Serikali Juma Kiparo, mtuhumiwa alitenda kosa hilo mnamo tarehe 16.08.2024 huko maeneo ya kijiji cha Shilima, wilaya ya Kwimba na mkoa wa Mwanza.

Mhanga ambaye jina lake linahifadhiwa kwa sababu za kisheria, alifanyiwa kitendo hicho wakati ameagizwa na mama yake dukani na wakati anarudi ndipo mtumiwa alimvuta nyuma ya nyumba ya baba wa mhanga kisha kumfanyia ukatili huo.

Mshtakiwa alifikishwa mahakamani tarehe 23.08.2024 na kusomewa shtaka la kubaka kinyume na kifungu cha 130 (1)(2)(e) na 131 (3) vya Kanuni ya Adhabu sura ya 16 ya Sheria marejeo ya mwaka 2022.

Mshtakiwa ameiomba Mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa yeye mwenyewe ni mgonjwa wa mapafu, ana watoto watano mmoja mlemavu na pia anamlea mdogo wake ambaye naye ni mgonjwa pia mkewe amemuachia mzigo mkubwa wa kulea hiyo familia ni kubwa.

Mshtakiwa licha ya kuomba mahakama impunguzie adhabu, hakimu Ndeko amesema kwamba mahakama hiyo imefungwa mikono kwani kifungu cha 131 (3) cha Kanuni ya Adhabu ambacho mtuhumiwa ameshtakiwanacho kinatoa adhabu ya kifungo cha maisha na hakijampa hakimu kubadili adhabu hiyo.

Hivyo, mahakama imemhukumu mtuhumiwa kwenda jela maisha. Hukumu hiyo imetolewa leo tarehe 20.11.2024 na hakimu mkazi mkuu Ndeko Dastan Ndeko ambaye ndio hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo baada ya kusikiliza mashahidi 5 wa Jamhuri akiwemo mhanga, mahakama imejiridhisha pasi na kuacha shaka kwamba mtuhumiwa ametenda kosa hilo.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka iliyosomwa na mwendesha mashtaka wa Serikali Juma Kiparo, mtuhumiwa alitenda kosa hilo mnamo tarehe 16.08.2024 huko maeneo ya kijiji cha Shilima, wilaya ya Kwimba na mkoa wa Mwanza.

Mhanga ambaye jina lake linahifadhiwa kwa sababu za kisheria, alifanyiwa kitendo hicho wakati ameagizwa na mama yake dukani na wakati anarudi ndipo mtumiwa alimvuta nyuma ya nyumba ya baba wa mhanga kisha kumfanyia ukatili huo.

Mshtakiwa alifikishwa mahakamani tarehe 23.08.2024 na kusomewa shtaka la kubaka kinyume na kifungu cha 130 (1)(2)(e) na 131 (3) vya Kanuni ya Adhabu sura ya 16 ya Sheria marejeo ya mwaka 2022.

Mshtakiwa ameiomba Mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa yeye mwenyewe ni mgonjwa wa mapafu, ana watoto watano mmoja mlemavu na pia anamlea mdogo wake ambaye naye ni mgonjwa pia mkewe amemuachia mzigo mkubwa wa kulea hiyo familia ni kubwa.

Mshtakiwa licha ya kuomba mahakama impunguzie adhabu, hakimu Ndeko amesema kwamba mahakama hiyo imefungwa mikono kwani kifungu cha 131 (3) cha Kanuni ya Adhabu ambacho mtuhumiwa ameshtakiwanacho kinatoa adhabu ya kifungo cha maisha na hakijampa hakimu kubadili adhabu hiyo.

Hivyo, mahakama imemhukumu mtuhumiwa kwenda jela maisha.

JELA MAISHA KWA KUBAKA MTOTO WA MIAKA 8 JELA MAISHA KWA KUBAKA MTOTO WA MIAKA 8 Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on November 20, 2024 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.