test

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UWEZESHAJI TAASISI ZA UMMA YARIDHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA BENKI YA TCB

Na Mwandishi Wetu.

KAMATI ya kudumu ya Bunge ya uwezeshaji Taasisi za umma imeridhishwa na utendaji kazi wa Benki ya Biashara Tanzania -TCB, huku ikiielekeza benki hiyo kuendelea kutoa gawio kwa serikali kuu ili fedha hizo zitekeleze miradi mingine ya kimkakati.
                               
Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam Leo na Mwenyekiti wa kamati hiyo Augustino Vuma wakati kamati hiyo ilipotembelea benki hiyo ili kufahamu mikakati, utendaji kazi pamoja na mwelekeo wake kwa mwaka 2025.

Amesema pamoja na mambo mengine ushirikiano wa benki hiyo na taasisi nyingine za serikali ikiwemo Shirika la Reli Tanzania -TRC, katika utoaji wa huduma imetajwa kuwa kichocheo muhimu cha ukuaji wa uchumi nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa -TCB, Adam Mihayo amesema benki hiyo itaendelea kushirikiana na serikali katika nyanja zote ikiwa ni pamoja na Kijamii na kiuchumi. 

" Tutaendelea kuchapa kazi kwa nguvu zote kwa maana serikali yetu ina matarajio makubwa na Taasisi hii kwasababu ni taasisi ya kimkakati kwa maana ni matarajio ya serikali yetu kwa taasisi hii kuongeza ujumuishwaji wa Kifedha ".

                                     

Itakumbukwa kuwa Kamati hiyo imekua ikifanya ziara yake ya kutembelea taasisi mbalimbali za Serikali ili kusikiliza changamoto zao, kuona utendaji wao wa kazi na kuwasilisha ripoti kwa serikali kuu.

                                 




          







KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UWEZESHAJI TAASISI ZA UMMA YARIDHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA BENKI YA TCB KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UWEZESHAJI TAASISI ZA UMMA YARIDHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA BENKI YA TCB Reviewed by Adery Masta on November 16, 2024 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.