test

TBS WATOA ELIMU YA UDHIBITI UBORA WA ZABIBU DODOMA , MAONESHO YA KIMATAIFA YA WAWEKEZAJI WA ZABIBU

                            

Afisa Udhibiti Ubora Mwandamizi  (TBS) Bi. Sifa Chamgenzi, akitoa elimu ya masuala ya udhibiti ubora kwa wananchi waliotembelea banda la TBS kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Wawekezaji wa Zabibu yanayofanyika katika Viwanja vya Mashujaa mkoani Dodoma.

Na Mwandishi Wetu.

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kutoa elimu kuhusu masuala ya udhibiti ubora kwa wananchi waliotembelea banda lao kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Wawekezaji wa Zabibu, yaliyofanyika katika Viwanja vya Mashujaa, mkoani Dodoma.


Katika maonesho hayo, Afisa Udhibiti Ubora Mwandamizi (TBS) Bi. Sifa Chamgenzi ameeleza umuhimu wa viwango vya ubora katika bidhaa za zabibu, huku akielezea jukumu la TBS katika kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa na kuuzwa nchini zinakidhi viwango vya ubora na usalama kwa matumizi ya wananchi.
Elimu hii ililenga kuongeza ufahamu kuhusu udhibiti wa viwango, na kusaidia wananchi na wawekezaji katika sekta ya zabibu kuelewa mchango wa TBS katika kukuza uchumi na biashara za kimataifa.
TBS WATOA ELIMU YA UDHIBITI UBORA WA ZABIBU DODOMA , MAONESHO YA KIMATAIFA YA WAWEKEZAJI WA ZABIBU TBS WATOA ELIMU YA UDHIBITI UBORA WA ZABIBU DODOMA , MAONESHO YA KIMATAIFA YA WAWEKEZAJI WA ZABIBU Reviewed by Adery Masta on November 28, 2024 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.