Na Mwandishi Wetu.
Dar es Salaam, 13 Desemba 2024: Safina Selasi Mgala anayefanya kazi za ndani wa Tegeta jijini ndiye aliyeibuka mshindi wa shilingi milioni 10 katika droo ya tano ya Kampeni ya Magift ya Kugift inayoendeshwa na kampuni ya mtandao wa simu ya Yas Tanzania.
Kufuatia ushindi Safina alikabidhiwa mfano wa hundi na kisha kuingiziwa kiasi hiyo cha pesa kwenye simu yake kupitia Mixx By Yas (zamani Tigo Pesa) katika hafla hiyo iliyofanyika Tegeta Nyuki jijini na kushuhudiwa na umati ulifurika eneo hilo.
Safina alijishindia kiasi hicho cha pesa kutokana na kutumia huduma za Yas ikiwemo kununua vocha, kufanya miamala mbalimbali kupitia Mixx By Yas ikiwemo malipo ya huduma za serikali, ikiwemo kulipa bili za maji, umeme, kutuma na kupokea pesa na huduma nyinginezo.
Kwa ushindi wa Safina jamii inajifunza kuwa ushindi katika kampeni ya Magift ya Kugift unaweza kumfikia mtu yeyote unachotakiwa ni kufanya juhudi kutumia huduma za Yas aliongezea kuwa pesa iyo ataitumia kufungua biashara ya Nguo.Kwa upande mwingine Makao Makuu ya Kampuni ya Yas , Zawadi mbalimbali za Fedha na Simu zilizotelewa ambapo Watumiaji wa mtandao wa simu wa Yas kupitia Kampeni yake inayoendelea ya Magift ya Kugift droo ya tano washindi watatu wamejinyakulia shilingi milioni moja kila mmoja.
Washindi hao walikabidhiwa hundi ya fedha walizojishindia na msemaji wa kampeni hiyo, Haji Manara maarufu kama Bugati.
No comments: