test

MAGIFTI YA KUGIFTI AWAMU YA PILI , FANYA HAYA NA USHINDE ZAWADI KIBAO KUTOKA YAS

Na Mwandishi Wetu.

Dar es Salaam, 5 Desemba 2024 – Kampuni inayoongoza ya mtindo wa maisha kidijitali nchini Tanzania, Yas, na Mixx by Yas, inayo furaha kutangaza kuanza kwa Awamu ya Pili ya kampeni yake maarufu ya mwisho wa mwaka, “Magift ya Kugift”. Kampeni hii, itakayodumu kwa wiki 13, inaadhimisha mabadiliko ya chapa kutoka Tigo kuwa Yas, na Tigo Pesa kuwa Mixx by Yas, ikifungua ukurasa mpya wa ubunifu na kuimarisha uhusiano na wateja, mawakala, na wafanyabiashara kote nchini.

                                  

Awamu ya Pili ya kampeni hii inajenga juu ya mafanikio makubwa ya awamu ya kwanza, ambayo tayari imewanufaisha zaidi ya wateja 150 na mawakala/wafanyabiashara 48 kwa zawadi za kuvutia. Katika msimu huu wa sikukuu, Yas na Mixx by Yas wameongeza msisimko zaidi kwa kutoa zawadi kubwa mbili za mwisho: gari jipya la KIA Sorento na kitita cha pesa taslimu cha Shilingi milioni 50 kwa mshindi mmoja wa bahati nasibu.

Tangu kuzinduliwa kwa kampeni hii, mwitikio kutoka kwa washiriki umekuwa wa kusisimua. Ndani ya wiki tatu pekee, wateja wamejishindia zawadi za pesa taslimu za kila siku za Shilingi milioni 1, simu janja, na zawadi za kila wiki za Shilingi milioni 5, huku mawakala na wafanyabiashara wakijinyakulia zawadi za pesa taslimu za kila wiki za Shilingi milioni 1.

Akizungumzia mafanikio ya kampeni, Angelica Pesha, Afisa Mkuu wa Mixx by Yas, alisema:

                            

“Magift ya Kugift ni ishara yetu ya shukrani kwa wateja na washirika wetu waaminifu wanaofanya Mixx by Yas kuwa ya kipekee. Tunapoingia Awamu ya Pili, tunafurahia kuleta fursa zaidi zinazobadilisha maisha kwa jamii yetu. Hii si kampeni tu, bali ni sherehe ya mshikamano na furaha ya pamoja, tunapofunga mwaka kwa kutoa shukrani kwa dhati.”

Kwa upande wake, Isack Nchunda, Afisa Mkuu wa Biashara wa Yas, alisema:

“Kampeni hii inaonyesha dhamira yetu ya dhati ya kuunda uzoefu wenye maana kwa wateja wetu. Kupitia Awamu ya Pili, hatutoi zawadi tu, bali tunaimarisha maadili ya uaminifu, mshikamano, na jamii ambayo yamekuwa msingi wa safari yetu. Tunawahamasisha wote kushiriki nasi kuufanya msimu huu kuwa wa kukumbukwa.”

Ili kushiriki, wateja wanapaswa kufanya miamala inayokubalika kupitia Mixx by Yas au kununua vifurushi vya Yas. Kila muamala unampa mteja nafasi ya kushinda zawadi za kila siku, kila wiki, na kila mwezi, na mwishowe kuingia kwenye droo kubwa ya kushinda KIA Sorento au kitita cha Shilingi milioni 50. Mawakala na wafanyabiashara pia wanastahiki kushinda kwa kufanikisha viwango vya miamala vilivyowekwa, ikiashiria dhamira ya chapa hizi katika kusaidia ukuaji na mafanikio ya washirika wao.

                           

Magift ya Kugift inaonyesha dhamira ya Yas na Mixx by Yas ya kuboresha sherehe za mwisho wa mwaka na kuwawezesha watu binafsi na jamii kwa zawadi zinazochochea matumaini na fursa mpya.

Kwa nafasi ya kushinda, fanya miamala na Mixx by Yas au nunua vifurushi vya Yas leo. Fanya msimu huu usisahaulike kwa kushiriki katika Magift ya Kugift – tuungane kusherehekea roho ya utoaji.












MAGIFTI YA KUGIFTI AWAMU YA PILI , FANYA HAYA NA USHINDE ZAWADI KIBAO KUTOKA YAS MAGIFTI YA KUGIFTI AWAMU YA PILI , FANYA HAYA NA USHINDE ZAWADI KIBAO KUTOKA YAS Reviewed by Adery Masta on December 05, 2024 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.