test

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU ASHANGAZWA NA VIPAJI VYA WANAFUNZI WA DIT KATIKA TEKNOLOJIA

 Na Mwandishi Wetu.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia anayeshughulikia masuala ya Sayansi Profesa Daniel Mushi ameipongeza Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kuzalisha vijana Mahiri  wenye ujuzi unaohitaji katika kujenga uchumi unaoakisi maendeleo ya Sayansi na Teknolojia.

                          

Ametoa pongezi hizo alipomuwakilisha Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda katika mahafari ya 18 Kundi la kwanza ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Kampasi ya Dar es Salaam.

                                     

Amesema DIT ni kiwanda cha kuzalisha wataalamu wenye weledi wanaotarajiwa kutumika katika sekta ya viwanda. Ametumia fursa hiyo kuwasihi Mashirika ya Umma na ya Kibinafsi kuwatumia  wahitimu hao wa ufundi sanifu, Teknolojia na Uhandisi aliowatambua kama  hazina kubwa kwa Taifa kuendesha miradi mikubwa ya kimkakati inayolenga kutoa matokeo chanya kwenye uchumi wa Taifa. 

"njooni sasa mchukue/mshirikiane na vijana hawa (Wahitimu 1463) katika kutatua changamoto zinazotusibu katika shughuli mbalimbali za kijamii na za kiuchumi"

Aidha, amewasihi wahitimu hao wa fani za ufundi stadi na Uhandisi  kutumia ujuzi walioupata kwa manufaa ya Jamii na Taifa kwa Ujumla na kujiepusha na matumizi mabaya ya ujuzi wao kufanya  maangamizi katika Jamii.

"Najua kwamba Elimu mliyoipata ni kubwa ninaomba tu kuwaasa mkaitumie kwa manufaa ya Jamii, kwa sababu najua mkiamua kutumia maarifa na ujuzi mlionao vibaya mnaweza mkaiumiza Jamii pia"

Pia amepongeza juhudi zinazochukuliwa na Menejimenti ya DIT kutoa nafasi kwa Walimu na watumishi wote kwenda kujiendeleza kielimu ili kuongeza ujuzi mpya unaoboresha maarifa wanayotoa kwa wanafunzi.

Vilevile ameipongeza DIT kwa kuwa na mashirikiano na Taasisi za Elimu za nje ya Nchi (China, Ethiopia, Urusi, Ufaransa, Uganda, Uturuki, Kenya, Korea, Hungary na Afrika kusini) kwa lengo la kuhakikisha wataalamu wanapata ujuzi na uzoefu unaoendana na  mahitaji ya kikanda na Kimataifa.


Akizungumzia Jitihada zinazochukuliwa na Serikali kuboresha Elimu na ufundi stadi na Uhandisi, Prof Mushi amesema Serikali imefanya imezijengea uwezo vyuo vya  ufundi stadi kuongeza udahili wa wanafunzi kutoka Wanachuo 171,851 hadi kufikia wanafunzi 235,804 sambamba na ongezeko la vyuo kutoka 465 hadi 474 kwa mwaka wa 2022/2023.


Sambamba na hayo Serikali imetoa mafunzo kwa wakufunzi 45 kutoka Taasisi za Elimu na mafunzo ya Elimu ya Ufundi stadi kwa lengo la kuongeza uwezo wa ufundishaji wa mitaala inayoendana na mabadiliko ya kiteknolojia na mahitaji ya soko.


Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Mhandisi Dkt. Richard Joseph Masika amesema lengo la kufanya mahafari hayo ni kuitangazia Umma bidhaa Bora ya wahitimu Mahiri katika kada ya uhandishi wanaozalishwa na DIT.

















NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU ASHANGAZWA NA VIPAJI VYA WANAFUNZI WA DIT KATIKA TEKNOLOJIA NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU ASHANGAZWA NA VIPAJI VYA WANAFUNZI WA DIT KATIKA TEKNOLOJIA Reviewed by Adery Masta on December 06, 2024 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.