Desemba 20 , 2024: Meneja wa TBS Kanda ya Mashariki Bi. Noor Meghji akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu ushiriki wa TBS katika Maonesho ya Nne ya Biashara na Uwekezaji Mkoa wa Pwani, yaliyofanyika Kibaha Mkoani Pwani Tangu Desemba , 17 - 20 , 2024 . Bi. Noor amesema TBS wameyatumia maonesho hayo kutoa elimu ya Viwango kwa Wafanya biashara , Wawekezaji na Wananchi ambapo TBS imehimiza umuhimu wa kuzingatia ubora katika uwekezaji ili kuwalinda wananchi.
Afisa Masoko Mwandamizi TBS Bi. Rhoda Mayugu ( kushoto ) akizungumza na baadhi ya wajasiriamali na wazalishaji wa Bidhaa kuhusu umuhimu wa kuwa na nembo ya Ubora ya TBS ambayo inatolewa Bure.
Na Adery Masta .
Desemba 20, 2024 , Shirika la Viwango Tanzania TBS limeshiriki katika maonesho ya Nne ya Biashara na Uwekezaji Mkoa wa Pwani , ambapo Shirika limetumia Maonesho hayo kutoa elimu kwa Wafanya biashara , Wawekezaji , na Wananchi kuhusu umuhimu wa kuzingatia Viwango .
Akizungumza katika Maonesho hayo yaliyofungwa rasmi Desemba 20 , 2024 Meneja wa TBS Kanda ya Mashariki Bi. Noor Meghji amesema
" TBS inahimiza kuhakikisha kwamba ubora unazingatiwa katika uwekezaji kwa sababu iwapo hujahakikisha ubora wa Mifumo , Bidhaa au ubora katika uwekezaji basi Viwanda , Biashara na Uwekezaji huo hauwezi kuwa endelevu na ndio maana tupo hapa kuwakumbusha na kuhamasisha masuala ya Viwango kwa sababu ni moja ya majukumu yetu " amesema Bi. Noor
Ikumbukwe Maonesho haya yalifunguliwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb), Desemba , 17 na yamefungwa hapo Jana Desemba 20 , 2024 na Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Hamis Ulega, ambapo alisisitiza dhamira ya serikali ya kuhakikisha miradi ya ujenzi wa barabara inakamilika kwa wakati ili kuboresha mazingira ya uwekezaji.
Katika hotuba yake, Mhe. Ulega alisema, "Serikali inatekeleza maagizo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha barabara zote muhimu mkoani Pwani zinajengwa haraka ili kupunguza msongamano wa foleni na kuwezesha wawekezaji kufanya biashara zao kwa ufanisi zaidi. TANROADS kwa sasa imeongeza kasi kwa kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha miradi hii kwa muda uliopangwa."
No comments: