Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza leo Disemba 27.2024 katika eneo la Usagara limeendea kudhibiti hali ya usalama barabarani kwa kufanya ukaguzi wa kushtukiza kwenye magari yanayobeba abiria kwenda mikoani kwa lengo la kuzui ajali zinaotokana na uzembe wa madereva.
Zoezi hilo limesimamiwa na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Mwanza, Mrakibu wa Polisi (SP) Sunday Ibrahim sambamba na kutoa elimu kwa abiria ambapo mbali na kuchukua hatua za kisheria pia amewakumbusha abiria haki zao za msingi na kuwataka kutofumbia macho vitendo viovu vinavyofanywa na baadhi ya madereva kwa kutoa taarifa Polisi.
Katika ukaguzi huo magari mawili yamekamatwa na wamiliki kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kushindwa kutimiza masharti/kanuni inayowataka kuajiri madereva wawili kwa mabasi yanayosafiri umbali mrefu wa zaidi ya masaa nane.
Kwa upande wao baadhi ya abiria wamelipongeza Jeshi la Polisi kwa kufanya ukaguzi wa kushitukiza na kuomba liwe endelevu kwani imebainika kuwa baadhi ya madereva wamekuwa wanafata sheria za usalama barabarani pale wanapowaona askari kitendo ambacho kinahatarisha maisha ya abiria na watumiaji wengine wa barabara.
"Zoezi linalofanywa na Jeshi la Polisi ni kwaajili ya usalama wetu sisi wananchi, sio vyema gari la mwendo mrefu likawa na dereva mmoja" amesema Donald Chakachaka (abiria)
"Nimelipokea zoezi hili kwa mikono miwili kwasababu linatusaidia sisi wasafiri kutuepusha na ajali kwahiyo nawapongeza Polisi wako sawa" amesema Mwajima Hamis (abiria)
Naye, dereva wa kampuni ya mabasi Nyehunge Hassan Maneno amesema vitendo vya uvunjaji wa sheria za usalama barabarani vimepungua kwa mkoa wa Mwanza
" Hakuna zile vurungu za kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari , tunazingatia mistali sana sana kwa hiyo nalipongeza sana jeshi la polisi kwa kazi nzuri wanayofanya " amezema Maneno
No comments: