KATONI ZA MIFUKO YA PLASTIKI ILIYOPIGWA MARUFUKU ZANASWA MWANZA.

test


JESHI la polisi mkoani Mwanza limekamata mifuko ya plasitiki katoni 1,162 iliyopigwa marufuku kutumika hapa nchini kutokana na kusababisha uharibifu wa  mazingira ikiwa inasafirishwa katika ziwa Victoria kuingizwa Jijini Mwanza. 


Kamanda wa polisi mkoani Mwanza Wilbroad Mutafungwa aliwambia waandishi Habari Leo Jijini Mwanza kuwa tatehe 12 mwezi huu katika eneo la Nyangulugulu kata na Wilaya ya Ilemela Stanslaus Weria (22) mfanyabiashara mkazi wa Kata ya Guta Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, Byabato Gidion (34) mvuvi na mkazi wa Misenyi Mkoani walikamatwa wakiwa na mifuko hiyo ya plasitiki.



Mutafungwa alisema mifuko hiyo 180,200 sawa na katoni 1162 ilikamatwa ikiwa kwenye mtunbwi MV Kabula 1 yenye namba za usajiri TMZ 01245 na upelelezi wa shauri hiyo ukiwa unaendelea kwa ushirikiano na Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Mkoani Mwanza.


Kamanda Mutafungwa ameonya dhidi ya matukio hayo ya kusambaza mifuko ya plasitiki ilizuiwa kutokana na kusababisha uharibifu wa mazingira.

KATONI ZA MIFUKO YA PLASTIKI ILIYOPIGWA MARUFUKU ZANASWA MWANZA. KATONI ZA MIFUKO YA PLASTIKI ILIYOPIGWA MARUFUKU  ZANASWA MWANZA. Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on February 20, 2025 Rating: 5

Post Comments

Powered by Blogger.