Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ilemela kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndg. *Kafiti William Kafiti,* leo Septemba 26, 2025 ametembelea Mwalo wa Igombe uliopo Kata ya Bugogwa, ambapo amekutana na kufanya mazungumzo na wafanyabiashara wa dagaa, pamoja na kusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili katika shughuli zao za kila siku.
Akizungumza na wafanyabiashara hao, ameahidi kuweka mazingira wezeshi ya upatikanaji wa mikopo ya asilimia 10% inayotolewa na Halmashauri, na kuwasihi kujiunga kwenye vikundi ili kukidhi vigezo vya kunufaika na mikopo hiyo.
Aidha, ameahidi kushirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kuhakikisha wananchi wa Bugogwa wananufaika na mikopo ya Maendeleo ya Wanawake pamoja na fursa nyingine za kiuchumi zinazotolewa na Serikali.
Amesisitiza dhamira yake ya kuendelea kushirikiana na wananchi wa Bugogwa katika kuinua uchumi kupitia sekta ya Uvuvi, kama nyenzo muhimu ya kukuza kipato kwa wananchi.

No comments: